JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Wakufunzi katika mafunzo hayo Mwl. Deus Kibamba ambaye ni Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia na Dkt. Ananilea Nkya ambaye ni Mkurugenzi Mstaafu wa TAMWA na Mwenyekiti wa Bodi ya Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Dkt. Ananilea Nkya, wamesema kwa sasa nchi inahitaji kupata katiba mpya ili kuenenda na wakati uliopo ambapo yapo mambo mengi hayako vizuri katika uwajibikaji.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa polisi ulioko Manispaa ya Mpanda huku makundi maalumu akihudhuria wakiwemo vijana, watu wenye ulemavu na akina wanawake.