Responded Dkt. Andrew: Tumetengewa Tsh. 800M ya kuboresha Miundombinu ya Hospitali ya Manispaa ya Singida

Responded Dkt. Andrew: Tumetengewa Tsh. 800M ya kuboresha Miundombinu ya Hospitali ya Manispaa ya Singida

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Singida, Dkt. Godfrey Andrew ameeleza kuwa Halmashauri ya Manispaa hiyo imetenga fedha kiasi cha Tsh. Milioni 800 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya maboresho ya miundombuni.

Ameeleza pia kutakuwa na maboresho ya njia zinazounganisha majengo katika Hospitali ya Manispaa ya Singida (zamani Hospitali ya Mkoa) ili kurahisisha kuwatoa wagonjwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine ikiwemo kutoka kwenye Jengo la Wazazi na Jengo la Dharura.

Ameongeza kuwa kwa jumla Halmashauri ya Manispaa ilipata Shilingi Bilioni moja ya ujenzi ya miundombinu mipya.

Kuhusu hospitali hiyo haikuwa na Jengo la Dharura na Jengo la Wamama Kujifungulia, pia miundominu mingi ilikuwa chakavu, kiasi hicho kimetumika kujenga majengo hayo ambayo yanatumika.

Pia soma ~ Hospitali ya Manispaa ya Singida iboreshe njia ya kupitisha wagonjwa kutoka jengo moja kwenda lingine
 
Back
Top Bottom