Mganga Mkuu wa Manispaa ya Singida, Dkt. Godfrey Andrew ameeleza kuwa Halmashauri ya Manispaa hiyo imetenga fedha kiasi cha Tsh. Milioni 800 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya maboresho ya miundombuni.
Ameeleza pia kutakuwa na maboresho ya njia zinazounganisha majengo katika Hospitali ya Manispaa ya Singida (zamani Hospitali ya Mkoa) ili kurahisisha kuwatoa wagonjwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine ikiwemo kutoka kwenye Jengo la Wazazi na Jengo la Dharura.
Ameongeza kuwa kwa jumla Halmashauri ya Manispaa ilipata Shilingi Bilioni moja ya ujenzi ya miundombinu mipya.
Kuhusu hospitali hiyo haikuwa na Jengo la Dharura na Jengo la Wamama Kujifungulia, pia miundominu mingi ilikuwa chakavu, kiasi hicho kimetumika kujenga majengo hayo ambayo yanatumika.