Dkt. Asha Rose Migiro: Amani na usalama ni nguzo za maendeleo jumuhishi

Dkt. Asha Rose Migiro: Amani na usalama ni nguzo za maendeleo jumuhishi

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Balozi Dkt. Asha Rose Migiro, Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Mipango na Mwenyekiti wa timu kuu ya kitaalamu ya uandishi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, amepongeza uteuzi wa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Nderiananga, akisema kuwa ni ushahidi wa jinsi serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inavyotambua na kuthamini mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya taifa.

Akizungumza katika mkutano wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wa Kuhakiki Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, uliofanyika Jumapili, Desemba 15, 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Dkt. Migiro amebainisha kuwa Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 imejikita katika misingi ya utawala, amani, usalama, na utulivu, huku ikiwajumuisha watu wenye ulemavu kwa namna ya kipekee.

Balozi Migiro ameeleza kuwa msingi wa Dira 2050 umejengwa juu ya nguzo tatu ambazo ni kujenga taifa jumuishi lenye ustawi, haki, na linalojitegemea; kuimarisha uwezo wa watu na maendeleo ya jamii, na kujenga uchumi imara, jumuishi, na shindani.

Amefafanua kuwa katika nguzo ya pili, kipengele cha tatu kimetoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu kwa kuweka mkazo katika hifadhi ya jamii jumuishi. Pia, kipengele hicho kinalenga kuhakikisha upatikanaji wa bima ya afya kwa wote, kutoa ulinzi dhidi ya uonevu na unyanyasaji, hususani kwa watoto, wanawake, na watu wenye ulemavu.

Balozi Migiro amesisitiza kuwa uhakiki wa rasimu hiyo unalenga kubaini mapungufu na kuyarekebisha, sambamba na kuongeza yale ambayo hayajajumuishwa. Amesema hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa makundi yote, hususani watu wenye ulemavu, wanajumuishwa ipasavyo katika mipango ya maendeleo.


 
Back
Top Bottom