DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 197
- 233
Dkt. Ashatu ameyasema hiyo leo Agosti 25, 2025 mara baada ya kukabidhiwa rasmi fomu ya uteuzi wa kugombea Ubunge na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kondoa, kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, mkoani Dodoma.
Makabidhiano hayo ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Amemshukuru kwa namna ya kipekee Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kumteua kupeperusha bendera ya chama katika uchaguzi huo.
“Nawashukuru kwa dhati viongozi wa chama changu kwa kuniamini tena. Najua bado nina deni kwa wananchi wa Kondoa, naahidi kulilipa kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa usiku na mchana.” amesema Dkt. Ashatu.