Dkt. Bagonza: Kama Rais anaitaka Katiba Mpya, kwanini tuipiganie?

Dkt. Bagonza: Kama Rais anaitaka Katiba Mpya, kwanini tuipiganie?

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Askofu Dr. Benson Bagonza wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Karagwe, akizungumza na Sauti Digital Ijumaa Julai 24, 2026 amehoji kuhusu kauli ya Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi kuhusu kuipigania KATIBA MPYA

Pia soma Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya

Mimi kila jibu huwa linazua swali, kwa mfano amesema Mhe. Rais anaitaka kwasababu imewekwa kwenye ilani.

Swali langu ni kama Rais anaitaka kwanini tuipambanie? Maana yake Makamu wa Rais amesema tuipambanie, tukomae sasa kama Rais anaitaka kwanini tuipambanie?

Swali la pili tunapambana na nani ili kuipata?"

"Swali la tatu, Makamu kusema ni jambo zuri lakini anaposema Rais anaitaka kwanini Rais hasemi moja kwa moja? Ndiyo amewahi kusema lakini kutokana na hali ilivyo, kumekuwa na kigugumizi juu ya hilo na nadhani ni wakati sasa Rais mwenyewe aseme kuliko wasaidizi wake." -
 
Back
Top Bottom