Dkt. Baruani Mshale auliza zile R NNE zinamaanisha nini katika mitizamo ya waTanzania

Dkt. Baruani Mshale auliza zile R NNE zinamaanisha nini katika mitizamo ya waTanzania

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,522
Reaction score
37,398
Dkt. Baruani Mshale mtaalamu bingwa anajikita kuuliza zile R4 kwa mtanzania ambaye siye mwanasiasa zina maanisha nini


View: https://m.youtube.com/watch?v=C9abritQeXE

Mada hiyo tunduizi ya Dr. Baruani Mshale aliitoa mbele ya kwenye Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa na wadau wa demokrasia, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam

Dr. Baruani Mshale anakwenda mbali kuhusu unyenyekevu ni kwa ajili ya wananchi kuwa wanyenyekevu kwa viongozi wanasiasa na siyo wanasiasa kuwa wanyenyekevu kwa wananchi

Kurunzi yake haikuacha kuimulikia Bunge na kujiuliza je bunge hili lina wawakilishi tuliowachagua au siyo na kama ni la bunge hili litaweza kupitisha sheria na marekebisho ya katiba kama wananchi wanavyo tumaini. Anauliza Dkt. Baruani Mshale baada ya kuwa kuna muswaada unapelekwa mwezi Oktoba 2023 kufanyia marekebisho ya sheria kadhaa.

Dkt. Baruani Mshale anazitazama kauli za amani, hii inamaanisha amani au kuwakandamiza wananchi kwa kisingizio cha amani na wala siyo kabisa kutafuta vitu vya kweli vitakavyojenga amani ya kweli

Kusifia na kutukuza yaani uchawa kwa sasa imekuwa moja ya tunu ya taifa ? Anauliza Dkt. Baruani Mshale ...

Dr. Baruani Mshale ni mkurugenzi wa kutoa elimu na stratejia wa shirika lisilo la serikali la TWAWEZA (Baruani Mshale (Director, Learning and Strategy) Team and Partners – Twaweza


Falsafa ya 4 R au R Nne hapo mwezi Julai 2023 imetimia mwaka mmoja tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipotambulisha falsafa yake ya R nne (4R) ambazo anazitumia kushawishi na pia zimedakwa na makada pia viongozi wa serikali kuwa ndiyo inatoa muongozo wa matamanio nchi iende vipi.

More info :

DARASA LA KATIBA KWA WATU MILIONI 61 KWA MIAKA MITATU NDIYO TATIZO


View: https://m.youtube.com/watch?v=WyCGGV88fbc
 
Je maneno ya wapinzani ni matusi au propaganda ya watawala kuwazuia watu kuongea

View: https://m.youtube.com/watch?v=sqpIvzmwzl4
Mzungumzaji mwanasiasa mkogwe Steven Wasira anajenga hoja kwa maoni kuwa kuna matusi katika siasa, je huo mtizamo ni wa kweli au ni namna ya kuwanyazisha saiti za wasioridhika na mfumo uliopo wa kisiasa. Kada huyu wa chama dola kongwe alishambulia mitizamo tofauti na ya CCM wakati wa Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa na wadau wa demokrasia
 
Back
Top Bottom