Dkt. Bashiru Ally kuwa tena Katibu Mkuu wa CCM?

Dkt. Bashiru Ally kuwa tena Katibu Mkuu wa CCM?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,171
Reaction score
23,996
Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Sir Harold Wilson aliwahi kusema, ''A week is a long time in politics''.

Katika historia ya Tanzania, Dkt. Bashiru Ally kama inavyododoswa kwa sasa kurudi tena kuwa Katibu Mkuu wa CCM atakuwa ni mmoja wa watanzania ambao utumishi wao wa umma unaweza kidogo kulinganishwa na Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa!

Historia inaonyesha Rashid Kawawa aliwahi kushika nafasi ya juu kabisa katika serikali lakini baadaye akaja kushushwa mpaka kwenye nafasi ya waziri asiye na wizara maalum katika utawala wa Mwalimu Nyerere. Fikiria Makamu wa Rais ambaye pia ni Waziri Mkuu anajikuta amekuwa waziri tu!

Najua kuna baadhi ya watu wasiokuwa na uelewa mpana wa kile kilichokuwa kikiendelea walikuwa wakimcheka Rashid Kawawa alipokuwa anashushwa kwenye vyeo.

Watu waliokuwa wakimcheka Rashid Kawawa hawana tofauti na wale wa sasa waliomcheka na wanaendelea kumcheka Dkt. Bashiru Ally bila kujua kinachoendelea ndani ya CCM!

Kikao cha Mkutano Mkuu wa CCM kinachoenda kukutana Mwezi mwishoni mwa mwezi huu au ujao kinaenda kutoa majibu ya uhakika kuhusu sababu ya Dr. Bashiru Ally kurudishwa tena CCM kama Katibu Mkuu wa CCM Taifa!

Ninajua kuna kundi la baadhi ya wanaCCM ambao fagio la uhakiki wa mali za CCM na safisha CCM liliwakumba kwa sasa wanafanya kazi kuhakikisha Dkt. Bashiru asirudi tena CCM kama Katibu Mkuu lakini Wazee wa CCM ambao ni Makamu Mwenyekiti wa CCM wa Bara na yule wa visiwani wamekubaliana na uamuzi wa Mwenyekiti ajaye wa CCM Taifa wa kulipeleka jina la Dkt. Bashiru katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ili likathibitishwe kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa.

Kuna watu watakuja na hoja wakisema, atakuwaje Katibu Mkuu wa CCM wakati ni Mbunge na kwa nini alipewa Ubunge? Jibu la swali hili lilishatolewa kwenye uteuzi wa Dkt. Abdallah Saleh Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye alikuwa mbunge wa kuteuliwa kabla hajateuliwa kuwa Balozi. Dkt. Bashiru akiwa Katibu Mkuu wa CCM itabidi ajiuzulu Ubunge wake kama alivyofanya Dkt. Possi.

Kwa wasiojua, Dkt. Bashiru asingeondolewa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi na kubaki mitaani bila sehemu ya ''kumuingizia kipato'' wakati akisubiri wenye CCM kumthibitisha! Njia iliyotumika ni kumpa ''ajira'' ya muda mfupi ambayo inajulikana kisheria ili kusubiri Mkutano Mkuu wa CCM na Kikao cha NEC ya CCM.

Kuna msemo usemao, Anayelia mwanzoni, mwisho hucheka kwa furaha na anayecheka mwanzoni, mwisho hulia!
 
Duh!

Kama ni kweli, hiyo maana yake ni nini?

Kwamba alikuwa ‘effective’ [sana] katika hiyo nafasi mpaka mwenyekiti mpya kaona ni bora amrudishe?

Ila, huu uzi usije ukawa ni uchuro maana Mama keshasema mara kadhaa sasa kuwa huwa anasoma yajiriyo kwenye mitandao ya kijamii na naamini JF ni moja ya hiyo mitandao.
 
Nadhani neno ''efective'' ni pana sana.

Kwa kifupi ameibadilisha sana CCM katika utendaji wake lakini vilevile alihakikisha mapato ya CCM yanakusanywa vizuri kutoka kwenye vyanzo vyake ambavyo vingine vilikuwa vinaishia kwenye mikono ya baadhi ya viongozi ndani ya CCM.
 
msemaji Ukweli

ukatibu ni nafasi ya utendji,kwa utulivu wa Bashiru chama kitaenda mbele.

ila uenezi mpeni "mzawa wa ccm"

tunataka mtu mwenye kukijua chama,aliyekiishi chama ambaye akisimama watu wote wanasema jembe hilo.
Nadhani hii nafasi ilikuwa inamfaa sana Nape Nnauye lakini akaamua kutafuta ''mshahara mkubwa zaidi'' na cheo cha Uwaziri kupitia ubunge!
 
Nadhani neno ''efective'' ni pana sana.

Kwa kifupi ameibadilisha sana CCM katika utendaji wake lakini vilevile alihakikisha mapato ya CCM yanakusanywa vizuri kutoka kwenye vyanzo vyake ambavyo vingine vilikuwa vinaishia kwenye mikono ya baadhi ya viongozi ndani ya CCM.
Effective = successful in producing a desired or intended result.

Kama alifanikiwa katika hayo uliyoyataja, basi hoja inaweza kujengwa kwamba alikuwa ‘effective’ kipindi akiwa katibu mkuu.
 
Effective = successful in producing a desired or intended result.

Kama alifanikiwa katika hayo uliyoyataja, basi hoja inaweza kujengwa kwamba alikuwa ‘effective’ kipindi akiwa katibu mkuu.
Siwezi kusema amefanikiwa katika malengo yote ya CCM lakini ninaweza kusema amefanikiwa katika mengi.
 
Ya CCM tuwaachie CCM
Wanajua nini wanafanya
Kabisa aisee, kama kuna visebengo flani wanavyoingilia mambo ya vyama vya upinzani tena hadi bungeni, huwa nawashangaa sana
 
Kwa wasiojua, Dkt. Bashiru asingeondolewa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi na kubaki mitaani bila sehemu ya ''kumuingizia kipato'' wakati akisubiri wenye CCM kumthibitisha! Njia iliyotumika ni kumpa ''ajira'' ya muda mfupi ambayo inajulikana kisheria ili kusubiri Mkutano Mkuu wa CCM na Kikao cha NEC ya CCM.
Kama kuna mtu alikuwa hajui maana ya uzandiki huu ndio uzandiki wenyewe. Yaani Bashiru kapewa ubunge wa mwezi mmoja ili ajipatie kipato? yaani mtu aliyekuwa KMK akose m11 ya kujikimu akisubiri mkutano mkuu umteue tena? I can’t buy this.
 
Back
Top Bottom