GE2025 Dkt. Bashiru: CCM ndio chama pekee chenye nguvu ya kupambana na rushwa

GE2025 Dkt. Bashiru: CCM ndio chama pekee chenye nguvu ya kupambana na rushwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mratibu wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa mikoa ya Kanda ya Kati, Dk Bashiru Ally, amesema CCM ndio chama pekee chenye uwezo wa kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Akizungumza Septemba 21, 2025, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Parking, Nzega Mjini, kwa ajili ya kuwaombea kura mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, pamoja na wagombea udiwani, Dk Bashiru aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi.

“Mmemsikia mgombea wetu wa urais alipokuwa Pemba amewataka wana CCM msikubali kuchokozeka, na siku ya uchaguzi mjitokeze kwa wingi kupiga kura kutakuwa na utulivu,” amesema Dk Bashiru, ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Aidha, aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso amesema mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, anastahili kuchaguliwa tena ili aendeleze mipango ya maendeleo aliyoianzisha.

“Katika kipindi chake aliposhika uongozi, tumeshuhudia kwa maneno na vitendo vya kimaendeleo kuanzia kwenye vijiji vyetu hadi Taifa kwa ujumla, pamoja na maridhiano ya kisiasa na kidemokrasia yaliyofungua milango ya siasa huru na wenzetu waliokimbia nchi walirudi,” amesema Paresso.

 
Back
Top Bottom