GE2025 Dkt: Bashiru: CCM ndio chama pekee chenye nguvu ya kupambana na Rushwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966

Mratibu wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa mikoa ya Kanda ya Kati, Dk Bashiru Ally, amesema CCM ndio chama pekee chenye uwezo wa kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Akizungumza Septemba 21, 2025, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Parking, Nzega Mjini, kwa ajili ya kuwaombea kura mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, pamoja na wagombea udiwani, Dk Bashiru aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi.

“Mmemsikia mgombea wetu wa urais alipokuwa Pemba amewataka wana CCM msikubali kuchokozeka, na siku ya uchaguzi mjitokeze kwa wingi kupiga kura kutakuwa na utulivu,” amesema Dk Bashiru, ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM. Aidha, aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso amesema mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, anastahili kuchaguliwa tena ili aendeleze mipango ya maendeleo aliyoianzisha. “Katika kipindi chake aliposhika uongozi, tumeshuhudia kwa maneno na vitendo vya kimaendeleo kuanzia kwenye vijiji vyetu hadi Taifa kwa ujumla, pamoja na maridhiano ya kisiasa na kidemokrasia yaliyofungua milango ya siasa huru na wenzetu waliokimbia nchi walirudi,” amesema Paresso.
 
Bashiru anaonge nini huyu mjuba? Hiyo ccm anailinganisha na chama gani kilichowahi kutawala kikashindwa kupanbana na rushwa? Kungekuwa na chama kilichowahi kutawala na kikashindwa kupambana na rushwa hapa ingekuwa sawa kukilinganisha na ccm katika mapambano ya rushwa
 
1758552734755.jpeg
... ngoja kwanza ...!
 
Hawa watu washatuona watanganyika ni mabogus ndio maana wanatuletea upuuzi daily.
 
Translation: CCM NDIO CHAMA PEKEE KINACHOJUA KUWAFICHA NA KUWATETEA WALA RUSHWA.
 
Mratibu wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa mikoa ya Kanda ya Kati, Dk Bashiru Ally, amesema CCM ndio chama pekee chenye uwezo wa kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Akizungumza Septemba 21, 2025, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Parking, Nzega Mjini, kwa ajili ya kuwaombea kura mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, pamoja na wagombea udiwani, Dk Bashiru aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi.

“Mmemsikia mgombea wetu wa urais alipokuwa Pemba amewataka wana CCM msikubali kuchokozeka, na siku ya uchaguzi mjitokeze kwa wingi kupiga kura kutakuwa na utulivu,” amesema Dk Bashiru, ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM. Aidha, aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso amesema mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, anastahili kuchaguliwa tena ili aendeleze mipango ya maendeleo aliyoianzisha. “Katika kipindi chake aliposhika uongozi, tumeshuhudia kwa maneno na vitendo vya kimaendeleo kuanzia kwenye vijiji vyetu hadi Taifa kwa ujumla, pamoja na maridhiano ya kisiasa na kidemokrasia yaliyofungua milango ya siasa huru na wenzetu waliokimbia nchi walirudi,” amesema Paresso.
Takataka nyingine kutoka jalalani
 
Hili boga linataka cheo tuu, sasa limeamua kuwa chawa tuu, na huyu si ndio alisema hatagombea nafasi nyingine yeyote baada ya kupewa ukatibu na Magufuli
 
Mratibu wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa mikoa ya Kanda ya Kati, Dk Bashiru Ally, amesema CCM ndio chama pekee chenye uwezo wa kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Akizungumza Septemba 21, 2025, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Parking, Nzega Mjini, kwa ajili ya kuwaombea kura mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, pamoja na wagombea udiwani, Dk Bashiru aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi.

“Mmemsikia mgombea wetu wa urais alipokuwa Pemba amewataka wana CCM msikubali kuchokozeka, na siku ya uchaguzi mjitokeze kwa wingi kupiga kura kutakuwa na utulivu,” amesema Dk Bashiru, ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM. Aidha, aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso amesema mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, anastahili kuchaguliwa tena ili aendeleze mipango ya maendeleo aliyoianzisha. “Katika kipindi chake aliposhika uongozi, tumeshuhudia kwa maneno na vitendo vya kimaendeleo kuanzia kwenye vijiji vyetu hadi Taifa kwa ujumla, pamoja na maridhiano ya kisiasa na kidemokrasia yaliyofungua milango ya siasa huru na wenzetu waliokimbia nchi walirudi,” amesema Paresso.
Madaktari wa siku hizi!! Hata naogopa kuitwa daktari!!1
 
Back
Top Bottom