Wakati nasoma chuo kikuu cha Dar es salaam enzi zile Hayati Dr.
Magufuli akimalizia masomo yake ya Shahada ya Uzamivu, nilimtambua Dkt Bashiru kama Msomi, Mzalendo, Mjamaa na mpenda mabadiliko ya dhati kwa maendeleo ya wananchi.
Kamwe sikutarajia kama IPO siku Dkt Bashiru atakuwa sehemu ya Chama tawala wala Serikali iliyopo madarakani maana viongozi wenzake wangempinga na kumtenga kutokana na imani na itikadi yake ya kuwakomboa watanzania kutoka katika umasikini, rushwa, maradhi na ujinga.
Naamini 100% kwamba Dkt Bashiru pia hakuwahi kufikiria kugombea vyeo vya kisiasa wala nafasi za uongozi.
Hulka yake, uzalendo wake na uchapa kazi wake ndizo tunu zilizomgusa JPM hadi kumuona kama msaada mkubwa katika kurudisha nidhamu ya chama na uwajibikaji wa chama kwa wananchi. Kazi hiyo aliifanya vyema na kurejesha nidhani, Hadji na sifa ya chama katika jamii.
Mafanikio ya Bashiru katika Chama, yalimuaminisha Mheshimiwa Hayati JPM kwamba Bashiru anafaa kuziba pengo LA katibu Mkuu Kiongozi
Hakika ni kwamba uteuzi wa Bashiru kushika Ukatibu Mkuu wa Chama, uliwashangaza wengi kama ambavyo pia uteuzi wa Bashiru kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ulivyowashtua wengi.
Leo hii, mheshimiwa Rais Samia ametengua uteuzi huo kwa kumteua katibu Mkuu Mwingine na Kumteua Dkt Bashiru kuwa Mbunge.
Mheshimiwa Bashiru, hiki ni kipimo cha ukomavu na weledi ndani ya kipindi kifupi.
Kuwa na moyo thabiti na utulivu wa nafsi na kukubaliana na hali. Endelea kuchapa kazi kwa weledi, usithubutu kuungana na kundi lolote, simamia msimamo wako.
Tambua pia kwamba, mabadiliko makubwa uliyoanzisha katika chama yamekujengea chuki na uhasama mkubwa kwa mafisadi ndani na nje ya chama. Unapaswa kuchukua tahadhari zote za msingi.
Baada ya mtikisiko mfupi, utazidi kuwa imara zaidi na nyota yako itang'ara. Kila LA kheri katika Majukumu yako ya Kibunge, saidiana na Mh. Polepole kukiimarisha chama na kumuunga mkono kwa dhati Mama Yetu Samia Suluhu Hassan. Uamuzi wake usikurudishe nyuma, Songa Mbele