Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru: Wagombea wa CCM kutoenguliwa ni suala la kutii Sheria

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amesema Wabunge na Madiwani wa CCM kutoenguliwa ni suala la kutii Sheria na kufuata Sheria.

Amesema, "Uchaguzi katika nchi zote unasimamiwa na Sheria na Kanuni. Tuna vitengo vya Sheria vinavyozunguka na kutowaruhusu Wagombea wetu wa ngazi yeyote kujaza fomu bila kuhakikiwa"

Ameongeza kuwa, suala la kukosea haliwezekani kwasababu CCM ni Chama cha Kitaasisi chenye mabalozi zaidi ya 250,000 ambao kazi yao kubwa ni kusimamia ushindi wa Chama.

Sikiliza mahojiano yake na BBC hapa:
Bashiru Ally: Uhuru ni kama njaa ukila unahitaji kula zaidi - BBC News Swahili
 
Hawa ndiyo aina ya wasomi tulio nao Tanzania, Bashiru, Kabudi, Lipumba, Kitila Mkumbo, Paschal Mayala, Polepole n.k wengine wengi, badala ya kusimamia ukweli na kulisadia taifa anaweka njaa zake mbele zaidi, walikuwa wanahubiri vitu ambavyo leo wao wenyewe wanaona aibu hata kuvikumbuka. Shame on them
 
Sasa si Wadanganyika tena,sasa ni WaTanganyika na mtaelewa ifikapo tarehe 28/10/2020 na mtapata taarifa tarehe 29/10/2020.
Na utanganyika wetu umetufanya tuchanganyike na kuwa kitu kimoja isipokuwa wachache ambao ni wenye meza na viti na wanafiki wa kidini ambao Mwenyezi Mungu anazidi kutudhihirishia na kuwajua ni nani yupo pamoja na wananchi na ni nani ni wanafiki ambao wanashindwa kuikemea batili inapotendwa na wenyeviti na meza wa CCM.
 
Hawa ndiyo aina ya wasomi tulio nao Tanzania, Bashiru, Kabudi, Lipumba, Kitila Mkumbo, Paschal Mayala, Polepole n.k wengine wengi, badala ya kusimamia ukweli na kulisadia taifa anaweka njaa zake mbele zaidi, walikuwa wanahubiri vitu ambavyo leo wao wenyewe wanaona aibu hata kuvikumbuka. Shame on them
Pascal Mayalla, ndiye msomi wa hovyo kuliko hoa wote! Maana hao wengine tayari wameokotwa Jalalani. Paskali akiokotwa Jalalani anaweza akaamua kutembea uchi kabisaaa.
 
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amesema Wabunge na Madiwani wa CCM kutoenguliwa ni suala la kutii Sheria na kufuata Sheria.

Amesema, "Uchaguzi katika nchi zote unasimamiwa na Sheria na Kanuni. Tuna vitengo vya Sheria vinavyozunguka na kutowaruhusu Wagombea wetu wa ngazi yeyote kujaza fomu bila kuhakikiwa"

Ameongeza kuwa, suala la kukosea haliwezekani kwasababu CCM ni Chama cha Kitaasisi chenye mabalozi zaidi ya 250,000 ambao kazi yao kubwa ni kusimamia ushindi wa Chama.

Sikiliza mahojiano yake na BBC hapa:
Bashiru Ally: Uhuru ni kama njaa ukila unahitaji kula zaidi - BBC News Swahili
Totally nonsense
 
Bashiru na Polepole ndio mfano wa watu wanaofanya taifa letu lisiende mbele.

Mmoja alikuwa mwanaharakati mwenye heshima yake ya kutosha, mwingine alikuwa mwalimu mwenye heshima ya kutosha.

Lakini angalia walipo sasa! Wameuza utu na heshima yao ili kupata mkate.
 
Hata kama tukitukana lakini hii issue ni muhimu kuifanyia kazi GRASSROOTS ni muhimu katika mikakati yote ya UShindi. Wenzetu wakipata viti wanahamia kwenye mitandao na kujenga mijini wakisubiri wakati wa uchaguzi ndo warudi kule. Kuna mgombea mmoja ambaye alisema kuwa aliomba wenzie wakawekeze kwenye mashina lakini walimpinga kichizi
 
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amesema Wabunge na Madiwani wa CCM kutoenguliwa ni suala la kutii Sheria na kufuata Sheria.

Amesema, "Uchaguzi katika nchi zote unasimamiwa na Sheria na Kanuni. Tuna vitengo vya Sheria vinavyozunguka na kutowaruhusu Wagombea wetu wa ngazi yeyote kujaza fomu bila kuhakikiwa"

Ameongeza kuwa, suala la kukosea haliwezekani kwasababu CCM ni Chama cha Kitaasisi chenye mabalozi zaidi ya 250,000 ambao kazi yao kubwa ni kusimamia ushindi wa Chama.

Sikiliza mahojiano yake na BBC hapa:
Bashiru Ally: Uhuru ni kama njaa ukila unahitaji kula zaidi - BBC News Swahili

Ati: Quote "Uchaguzi katika nchi zote unasimamiwa na Sheria na Kanuni. Tuna vitengo vya Sheria vinavyozunguka na kutowaruhusu Wagombea wetu wa ngazi yeyote kujaza fomu bila kuhakikiwa"Quote

Uchaguzi wa 1995,2000,2005,2015 miaka yote hii ilikuwa hamna sheria?
 
Pascal Mayalla, ndiye msomi wa hovyo kuliko hoa wote! Maana hao wengine tayari wameokotwa Jalalani. Paskali akiokotwa Jalalani anaweza akaamua kutembea uchi kabisaaa.
Pascal ni Msomi sasa? Msomi hujipambanua Kwa hoja zake. Pascal anajenga hoja kama mwanaKazura Mimba utamwita Msomi? Msomi hutetea taaluma yake hayumbishwi na njaa.

Ukiona mtu anaikana taaluma yake na kuamua kuongea tofauti Ili tu aweze kuishi basi jua hapo kuna Msomi Njaa. Pascal ni kundi moja na Polepole pamoja na Bashiru.
 
Nimemsikia akiongea BBC asubuhi, anaongea kwa ukali kama jana usiku aligombezwa na jiwe.
 
Hawa ndiyo aina ya wasomi tulio nao Tanzania, Bashiru, Kabudi, Lipumba, Kitila Mkumbo, Paschal Mayala, Polepole n.k wengine wengi, badala ya kusimamia ukweli na kulisadia taifa anaweka njaa zake mbele zaidi, walikuwa wanahubiri vitu ambavyo leo wao wenyewe wanaona aibu hata kuvikumbuka. Shame on them
Dawa ya mnafiki ni kumpuuza

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom