Ambition plus
JF-Expert Member
- Feb 23, 2018
- 6,101
- 11,381
Transformer 50-60 kuungua kwa mwaka hio ni uwongo..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wilaya hiyo ina changamoto ya radi nyingi zinazosabababisha transfoma kuungua kwa takriban 50 hadi 60 kwa mwaka
We Chizi nini, sisi tumezizoea hizo Porojo.Mungu mwema.Bwana asema mimi ni nuru atakayenifuata hataingia gizani milele.
Juzi kasema ni mgao endelevu, sijui kasahau?Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewaagiza wataalam kufanya ukarabati wa miundombinu ya umeme kwa wakati ili kuwawezesha wananchi kupata huduma ya umeme ya uhakika.
Dkt. Biteko amesema tabia ya kutobadilisha au kukarabati miundombinu kwa wakati pale inapoharibika inawakosesha wananchi huduma ya umeme kwa kipindi kirefu.
Amesema hayo tarehe 21 Februari, 2024 wakati wa ziara yake mkoani Njombe ambapo amewasha umeme katika Kijiji cha Ikwavila na Shule ya Sekondari ya Wasichana Njombe iliyoko wilayani Wanging'ombe pamoja na kukagua mindombinu ya uzalishaji umeme na nguzo za umeme katika kiwanda cha TANWAT.
Dkt. Biteko ametoa maagizo hayo baada ya Mbunge wa Wanging'ombe, Mhe. Dkt. Festo Dugange kueleza kuwa, Wilaya hiyo ina changamoto ya radi nyingi zinazosabababisha transfoma kuungua kwa takriban 50 hadi 60 kwa mwaka lakini ubadilishaji wake umekuwa ukichukua muda mrefu na hivyo kuathiri shughuli za kijamii na kiuchumi.
"Hili suala la transfoma inaungua halafu inachukua hadi mwezi mmoja kubadiliswa, uzembe huu haukubaliki, Idara ya Manunuzi TANESCO tumeibadilisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kama hii ya uzembe wakati vifaa hivi vinazalishwa kwenye viwanda vya ndani, tunataka watendaji hawa waone shida wanazopata wananchi na kuzitatua, kweli kuna changamoto ya umeme lakini kuna baadhi ya matatizo TANESCO wanaweza kuyamaliza." Amesema Dkt. Biteko
Amesema kuwa, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan hataki kero ya umeme iendelee ndio mana utekelezaji wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JHNPP) unaenda kwa kasi na sasa umefikia asilimia 99 na mtambo mmoja umekamilika utakaoingiza megawati 235 kwenye gridi mwezi huu huku mtambo mwingine ukitarajiwa kuingiza megawati nyingine 235 mwezi Machi mwaka huu.
Kuhusu ombi la Mbunge wa Wanging'ombe kupata laini ya umeme inayojitegemea kwani laini ya sasa inatumiwa pia na eneo Lupembe na TANWAT mkoani Njombe na hivyo kufanya umeme wilayani humo kuwa hafifu, ameagiza TANESCO kujenga kituo cha kupoza umeme wilayani humo ili kutengemaza hali ya upatikanaji umeme..