Charles Kimei hajulikani jimbo la vunjo na Kitendo cha halmashauri Kuu ya Kamati kuu ya CCM kukata Jina la inock koola zadock mtoto wa Tajiri wa kimarangu Mzee Koola(Mmiliki wa makampuni ya Zadock A1outdoor Africa), ambaye alishinda kura Za maoni imeigawanyisha CCM jimboni vunjo pande mbili, wanao muunga mkono kimei na wale walichukizwa na kitendo cha koola kukatwa. Palikuwa hakuna shamrashara kimei alivyotangazwa kama mgombea wa ubunge CCM vunjo. Pili, kulazimishwa kustaafu CRDB, wananchi wa vunjo wanajua Magufuli alishauri astaafu kuliko kutumbuliwa kwa kashfa ya kulipwa mil 45 kwa mwezi. Hawa ndio wale waliomchukiza magufuli kwa kulipwa zaidi ya mil 40 kwa mwezi na alisema hadharani.
James Mbatia alivyoshinda ubunge 2015 alilikacha jimbo na hakufanya kitu na alikuwa anaonekana kwa nadra sana jimboni humo. Alichangisha kila kaya 20,000 Za kuchonga barabara Jambo ambalo halikulitekeleza na limewaudhi wananchi jimboni humo. Jambo jingine ni kwamba mbatia ushindi wake wa 2015 ulibebwa na ukawa na dhana kwamba lowassa angekuwa Rais na mbatia kuwa waziri lakini hicho kitu hakipo kwa sasa kila chama kinajigemea hata Chadema ilimsaidia ashinde 2015, mwaka huu wameweka mgombea grace kiwelo.
Mrema ana historia ya uchapa kazi nzuri vunjo na kitendo chake cha kuwa karibu na kumuunga mkono Rais, Dkt. Magufuli kitampa kura kwa sababu ya imani kubwa wananchi walionayo kwa Mhe. Rais kwamba anafanya kazi nzuri. Mrema ameshafanya kazi na Magufuli miaka ya 2010 - 2015 ambapo magufuli alikuwa waziri wa ujenzi na Mrema mbunge wa vunjo walishirikiana kujenga barabara jimboni humo. Mrema kuteuliwa tena kuwa mwenyekiti wa bodi ya parole kwa kipindi cha pili 2020 - 2023 ni heshima kubwa aliyopewa na magufuli na yeye pekee yake kaingia kugombea ubunge bado kashikilia cheo alichopewa na Rais wengine wote wenye tamaa walitumbuliwa.Miradi mingi ya maendeleo ambayo alianzisha Mrema ilikufa baada ya Mbatia kuteuliwa wananchi wengi wanataka hiyo miradi irudi na anayeweza kuifufua ni Mrema. Mfano barabara Kawawa-nduoni-kilema-marangu mtoni. Kipindi cha ubunge wa Mrema paliwekwa lami marangu mtoni mpaka kilema na kawawa mpaka nduoni. Lakini Mbatia alivyoingia kwenye ubunge lami hiyo haijaunganishwa nduoni mpaka kilema.
Mrema ndio Mbunge wa vunjo