Dkt. Charles Kitima na Dkt. Slaa wote wamewahi kuwa Makatibu wa TEC haya ndiyo maoni yangu kuhusu waraka wa TEC

Mkuu, una elimu yoyote? Maana, hujui hata kama lile la jana ni Tamko la nani. Jua kuwa lile ni Tamko la Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania.

Padre Charles Kitima yeye ni Katibu wa Baraza hilo. Ametimiza tu majukumu yake ya kuliweka wazi kwa umma.

Mbona hata Tamko lenyewe linajionesha wazi na waliohusika nalo wamejitaja? Bure kabisa!
 
una akili sana hii reasoning inayotakiwa. wengine akiongea askofu baasi wanaaacha kufikiria
 
Chambua basi kuhusu hasa kilichoandikwa ndani ya hilo tamko, maana umejikita kumshambulia zaidi Kitima na Slaa binafsi zaidi ya hoja zao.
 
Acha kukariri we poyoyo, huwezi kuwa na akili kuliko majaji wa mahakama kuu
 
Ungejibu hoja za waraka ungeonekana mtu makini Ila kwakuwa umekuja kujadili kuhusu kitima Basi wewe ni zwazwa....
 
1. Tatizo la maoni yako linaanzia ktk kujadili watu (Dr Slaa & Kitima) badala ya kujadili hoja za TEC. Kwa hili tu maoni yako yanakuwa ya kimbea zaidi na yasiyojengwa ktk hoja za kimkataba na hivyo ni ya kupuuzwa moja kwa moja...

2. Pamoja na hayo, mimi nitakujibu kwenye maeneo kadhaa kuonesha upogo wa kufikiri kwako.
Kwanza tamko limesomwa na mtu mmoja bila kuwepo na askofu mwingine yeyote.
Kwa maana hiyo ungeweza kuelewa na kuona si "tamko la kidini" kama unavyosema hapo chini iwapo maaskofu wote wangeenda kusoma tamko hilo?. Hii ni hoja dhaifu na pengine ya kijinga tu..
Aliyesoma na kuandika tamko amekuwa miongoni mwa watu wanaopinga mkataba wa bandari kwa nyakati tofauti hata kabla ya tamko la leo.
Hakuna shida ktk hili. Muhimu ni kuangalia hoja ni za msingi ama la..
TEC imetumika kama Jukwaa lilisaidia Slaa na Kitima kufikisha hoja zao.
Hakuna shida. Ni Kama vile tu JF JUKWAA LA SIASA inavyokusaidia wewe wewe hapa kufikisha ujumbe au maoni yako. Kuna ubaya gani hapo?
Rejea mjadala mdaharo uliowashirikisha Rostam, Kitila Mkumbo, Zitto, Lema, Shekh Ponda, Balile na Dkt. Kitima mwenyewe.
Kwenye madahalo watu wote walikubaliana kuhusu umuhimu wa uwekezaji..
Exactly. Kama ambavyo sisi wengine wote tunaokubaliana kuwa uwekezaji wa ndani na kutoka nje ya nchi ni muhimu.

Kinachopingwa ni aina hii ya mikataba ya kilevi kama huu wa DP World kwa bandari zetu za Tanganyika..
Anatoa tamko kwamba TEC inapinga uwekezaji na wanamuamuru Rais Ufute mkataba.
Wewe ni mwongo!!

Soma vyema tamko la TEC uelewe kabla ya kuja kupotosha hapa. TEC haijapinga uwekezaji. Inapinga mkataba wa uwekezaji ktk eneo moja tu la Bandari za Tanganyika na waarabu wa Dubai Emirate kupitia kampuni yao ya DP World kwa sababu ni wa hovyo na usio na manufaa yoyote kwa nchi yetu...

TEC wako very professional unlike you ambaye unamwaga hoja za umbea wa kuokoteza mitaani tu bila kuwa supported na evidence toka kwenye kinacholeta shida yaani mkataba wa bandari. TEC imejenga hoja za kutokukubaliana Kwa kutumia yaliyomo kwenye mkataba wenyewe..!

Kwa kifupi sana ni kuwa ni kana kwamba viongozi wa serikali yetu wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan walikuwa wamelewa mvinyo wa kiarabu wakati wanaingia makubaliano haya ya kipuuzi na kijinga mtupu..!
Hoja ya kitoto nyingine hii. Mkataba wa TICTS uko sawa na huu wa Dubai/DP World? Mwenyewe umetaja muda wa TICTS ni miaka 22. Cha ajabu hujui kuwa wa DP World hauna ukomo!!

Ili tujadiliane vizuri, hebu weka mkataba wa TICTS tulinganishe na huu wa DP World ndo utajua kuwa kumbe hujui..!!
Hapa Kitima ni kama ana msalahi binafsi anayoyapigania kwa kutumia mwamvuli wa TEC, hoja yake inamashaka.
Kama yapi vile? Mbona hoja za TEC ziko very clear kiasi cha hata mjinga anaweza kuelewa? Wewe una shida gani?

Ingalau basi ungeyataja hayo maslahi binafsi ya Kitima labda ungetia uzito kidogo kwenye hoja yako
Kumbukeni sakata la ESCROW kuna hadi viongozi wa dini ambao walinufaika na wizi wa ESCROW sio wasafi kwa kiwango hicho.
Kitima alkuwemo?

By the way, unadhani hii ni hoja ya kuhalalisha mkataba huu?
Huu ni uthibitisho kuwa Kitima na Slaa ni wadini sana ambao Kuingia kwa Rais Samia madarakani kwao waliona ni suprise.
Haa haa, 🥱🥱🥱🥱, ni kama uko confused vile..

Na kama wao ni wadini, basi hata wewe ni mdini kwa sababu tu umetoa maoni yako juu ya bandari..
Kwa msingi huo, huu ni uthibitisho kuwa Tamko lililoitwa la TEC lina msukumo wa kidini kuliko msukumo wa kisheria na kisiasa.
Tena umerudia ishu ya udini. Jikite kwenye hoja za mkataba achana na dini za watu..

Ndugu Mpangawangu, TEC wametoa hoja zao reference ikiwa ni mkataba wa bandari. Wewe unajenga hoja zako kutoka wapi?
Je na waislaam nao wakitoa tamko lao linalopingana na tamko la TEC?
Inakubalika. Wao watoe tu kwani mwisho wa siku watu tunapima ukweli na uongo wa hoja na siyo maneno matupu. Hili wewe limeshakushinda maana unamwaga upupu wa maneno matupu tu bila hoja ndani yake..
Vipi walokole nao wakiunga mkono uwekezaji, serikali itafuata msimamo wa dini gani?
Soma hapo juu☝️☝️

Watoe tu tamko iwe ni kupinga au kukubaliana. Mwisho siku tunapima hoja na sio kelele tupu kama zako..

Huu ndiyo uhuru wa maoni ili mradi mtu hsvunji sheria..!!
Tumeshatoa maoni,serikali imeyasikia na ndani ya serikali kuna watu wa dini zote na wasiokuwa na dini, kuna wanasheria kuna vyombo mbalimbali vya dola.
Imeyasikia wapi wakati mkataba uko umeshasainiwa na kupitishwa (ratified)na bunge? Hayo maoni yaende wapi na kufanya nini? Unaelewa hata unachokisema kweli wewe??
Ni imani yangu kuwa Swala la uwekezaji wa Bandari watalifanyia kazi kwa kulinda maslahi ya taifa.
Kazi ni kufuatilia mbali uchafu huu. Mkataba huu hautufai. Serikali iachane na hii kitu mara moja kuepusha shari na vurugu kama ambavyo polisi walishaanza kuanzisha ili kuwatetea watawala wa CCM waliofanya upuuzi na kutuletea uchafu huu nchini kwetu..

The only way ni kuzingatia ushauri wa walio wengi (umma) wakiwemo TEC.

Hakuna anayepinga uwekezaji si ktk eneo la bandari tu bali kwenye sekta zote ili mradi mambo yafanyike kwa njia shirikishi kwa umma, kwa uwazi na kwa kuzingatia sheria na katiba ya nchi..
Viongozi wa dini wasiingile utendaji wa serikali ambayo kila mmoja anatambua haina dini.
Viongozi wa dini ni wananchi kama ulivyo wewe. Kusema au kutoa ushauri na maoni juu ya uendeshaji wa nchi yao huwezi kusema "wanaingilia utendaji wa serikali". Ni jukumu la serikali kuheshimu maoni ya Kila mtu..

Viongozi wa dini wakikaa kimya huku serikali ikitenda mambo mabaya na ya ajabu Kwa wananchi, Mungu wa mbingu na nchi hawezi kuwaelewa...

Kusema makosa ya viongozi wa serikali ili ijirekebishe na kutenda haki, ni utumishi wa Mungu uliotukuka Kwa watu watumishi wa Mungu wote..

Waambie hata hao mashekhe wa kiislamu nao waseme. Wakemee uovu na wapongeze palipo na haki..
Tuwapuuze Slaa na kitima, wanataka kutuingiza kwwnye vita yao ya maslahi binafsi kwa Kisingizio cha kulinda rasilimali ,
Wapuuze wewe maana ni haki yako ya kikatiba kumuunga au kutomuunga mkono mtu yeyote..

Sisi wengine tuko na umma wote wa Tanganyika unsopinga ujinga huu wa viongozi wa serikali hii isiyo na uhalali wa kisiasa toka kwa wananchi...!!

L
 
Mahakama imeshaamua kuwa mkataba hauna dosari,uendelee sasa kati ya TEC na Mahakama mnataka tufuate ya nani?
 
Wao wamesema wapo na wananchi hawajasema mfuate tamko lao ila utambue tu, TEC ilikuwepo kabla ya CCM, Tanganyika na Tanzania. Ilianzishwa 1957. Narudia tena sio lazima ufuate.
 
Nsha yako tumeiona kuhusu kitima na Slaa, sasa turudi kweny hoja za Tec!! Niliwaambia humu hili tamko la Tec litawatoa watu mapangoni kila mmoja atakuja na lake, na bado!! Nenda kale kwanza 👇👇👇
 

Attachments

  • IMG_20220928_154551.jpg
    44.8 KB · Views: 2
Tujibu hapa kwanza
 
Kama huamini hilo ni tamko la maaskofu kupitia katibu wao mkuu Kitima, ya kwamba ni utashi binafsi ,natarajia maaskofu wajitokeze kuukana,wasipojitokeza imekula kwako na walionyuma yako
 
Mahakama imeshaamua kuwa mkataba hauna dosari,uendelee sasa kati ya TEC na Mahakama mnataka tufuate ya nani?
Mahakama zetu hizi ni kwamba wananchi hawana njia nyingine ya kufuata. Lakini si za kutoa haki.

Ref: mweka hazina mstaafu wa ccm T (R. Aziz) . Just one call from government high ranking official, na Haki huipati. Angalia hata kilichoperekea kuchelewesha hukumu na ziara ya namba moja mbeya. Utaelewa na kama huelewi basi wewe ni mshabiki, na si mchunguzi.

Maghufuli aliwahi kusema mihimili hata kama inajitegemea lakini kuna uliojichimbia zaidi. Na akawaambia majaji kwenye siku ya sheria duniani. Fedha ninawapa lakini serikali isiwe ya kushindwa kila kesi inayowasilishwa mahakamani.
 
Mahakama imeshaamua kuwa mkataba hauna dosari,uendelee sasa kati ya TEC na Mahakama mnataka tufuate ya nani?
Mahakama zetu hizi ni kwamba wananchi hawana njia nyingine ya kufuata. Lakini si za kutoa haki.

Ref: mweka hazina mstaafu wa ccm T (R. Aziz) . Just one call from government high ranking official, na Haki huipati. Angalia hata kilichoperekea kuchelewesha hukumu na ziara ya namba moja mbeya. Utaelewa na kama huelewi basi wewe ni mshabiki, na si mchunguzi.

Maghufuli aliwahi kusema mihimili hata kama inajitegemea lakini kuna uliojichimbia zaidi. Na akawaambia majaji kwenye siku ya sheria duniani. Fedha ninawapa lakini serikali isiwe ya kushindwa kila kesi inayowasilishwa mahakamani.
 
Ufafanuzi mzuri
 
Kwa mada zinazoendele ni as if bandari iliuzwa na waislamu!
Kweli kukosa akili ni ugonjwa mbaya sana kwa waislamu wasiojielewa!
Amkeni enyi watu acheni mambo kipuuzi kiasi hiki! Hadi ccm inawacheka na kuwadharau!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…