Nimesoma tamko la TEC
Kwanza tamko limesomwa na mtu mmoja bila kuwepo na askofu mwingine yeyote.
Aliyesoma na kuandika tamko amekuwa miongoni mwa watu wanaopinga mkataba wa bandari kwa nyakati tofauti hata kabla ya tamko la leo.
TEC imetumika kama Jukwaa lilisaidia Slaa na Kitima kufikisha hoja zao.
Rejea mjadala mdaharo uliowashirikisha Rostam, Kitila Mkumbo, Zitto, Lema, Shekh Ponda, Balile na Dkt. Kitima mwenyewe.
Kwenye madahalo watu wote walikubaliana kuhusu umuhimu wa uwekezaji, Kitima pekee ndie alikuwa na hoja tofauti, akasema haoni sababu ya kukabidhi uhuru wetu kwa waarabu, akapinga uwekezaji na kutaka mkataba tuachane nao, tuwaachie vijana wa kitanzania waendeshe, akaongeza kuwa hata wakiiba watatumia pesa hizo humuhumu nchini(ingia youtube andika mdaharo wa bandari utaona ninachokisema)
Leo ameibuka kama katibu wa TEC nafasi iliyowahi kushikwa na Dkt. Slaa.
Anatoa tamko kwamba TEC inapinga uwekezaji na wanamuamuru Rais Ufute mkataba.
Kwenye andiko lake ametoa hoja kubwa tatu.
1. Kwenye andiko lake anadai Mihimili iheshimiane, isiingiliwe hapa alimaanisha Kesi ya Mwabukusi ambayo kwa vyovyote Kitima alihusika kuifungua.
Kushindwa kwa Mwabukusi ni sawa na kushindwa kwa Kitima, lazima Kitima atafute plan B.
Kitima kwenye andiko lake anasema mihimili isiingiliane, kila muhimili uwe huru.
Kwake anaamini walishindwa kesi kwakuwa mahakama haikuwa na uhuru wa kufanya maamuzi, Kitima ni kama anasema mahakama ilishinikizwa kutoa yale maamuzi.
Halafu anafanya makosa kwenye andiko hilohilo kuhusu hoja hiyo kwa mushinikiza Rais Samia kutengua maamuzi ya bunge ambao ni muhimili mwingine wa dola ambao awali amesema mihimili isiingiliwe.
Hapa anahalalisha kuingiliwa kwa munimili wa Bunge ili kufanikisha malengo yake.
Rais akiingilia bunge atakuwa naendelea kuvunja katiba, kukosea kwa kufanya kile ambacho Kitima anapinga kwenye Tamko lake.
2. Kuhusu hoja ya kutaka Bandari iendeshwe na wazawa, kwamba haijawahi kuendeshwa na wageni, amesahau kuwa Bandari imeendeshwa na TICS kwa miaka 22 hakulisema hili kwa makusudi, huenda anatamani TICS ndio iendelee badala ya DP-World ili kulinda maslahi binafsi aliyonayo bandarini.
Hapa Kitima ni kama ana msalahi binafsi anayoyapigania kwa kutumia mwamvuli wa TEC, hoja yake inamashaka. Kumbukeni sakata la ESCROW kuna hadi viongozi wa dini ambao walinufaika na wizi wa ESCROW sio wasafi kwa kiwango hicho.
3. Kitima na Dkt. Slaa ni watu wenye Itikadi kali ya ukristo(Udini)
Kuna Wakristo wasiokuwa na ubaguzi halafu kuna Slaa na Kitima waliopea kwenye Udini.
Sio utamaduni wetu Watanzania kunadiliana habari za udini ma Ukabila, lakini kwa muktadha huu nitalisemea ili muwajue vizuri.
kwa nyakati tofauti Kitima ameonesha ni mtu mwenye chuki ya kidini na mdini sana tangu akiwa Makamu mkuu wa chuo cha St Augustine Mwanza.
Nakumbuka wakati wa utawala wa Rais Kikwete kwenye kipindi cha star TV chini ya Dotto Bulendu kitima aliilaumu serikali ya Rais Kikwete kwa kuruhusu waarabu wenye ndevu hadi kifuani kuzagaa Kariakoo, alisema kwamba wale wenye ndevu ndio magaidi kwamba serikali inawatazama haiwachukulii hatua.
Yaani kwenye ule mjadala, kitima akaona ndevu ni tishio kwake.
Ndiyo maana Tangu utawala uchukuliwe na Rais Magufuli, Mkatoliki mwenzake Kitima hajawahi kujitokeza hadharani kuipinga serikalinya magufulipamoja na chamgamoto zote za Utawala wa Magufuli.
Kadhalika Dkt. Slaa, kwenye utawala wa Magufuli hakuwahi kuishambulia serikali kwa lolote hata pale palipokuwa na makosa ya wazi, baadae Slaa alipewa zawadi ya cheo kuwa balozi wa tanzania kwa kazi nzuri ya Kuhujumu demokrasia yetu.
Baadae alirudishwa nyumbani baada ya kumaliza muda wake wakati wa utawala wa Rais samia, hadi hivi karibuni kwenye sakata la mbowe, Slaa alisema mbowe anaweza kuwa gaidi kwamba mashtaka aliyoshtakiwa nayo yalikuwa halali, hapa alitoa kauli ya kumfurahisha Rais samia kwa lengo la kuwinda zawadi ya cheo kipya.
Rais Samia amejipambanua kuwa hataki wapambe ni kiongozi anaetembea kwenye 4R, msisitizo ukiwa mwafaka wa kitaifa.
Watu kama slaa ambao wanashangilia mauaji na uonevu Rais samia aliona hawawezi kumsaidia.
Pia Rais Samia anaamini katika uongozi wa vijana.Slaa ana zaidi miaka 78.
Baada ya Slaa kukiridhisha kuwa utawala wa Rais Samia hauna mpango wa kumtumia, ndipo akaamua kuungana na Dr.Charles Kitima kuishambukia serikali
Kama Slaa angepewa cheo, muda huu angekuwa anatetea Mkataba wa DP World.
Huu ni uthibitisho kuwa Kitima na Slaa ni wadini sana ambao Kuingia kwa Rais Samia madarakani kwao waliona ni suprise.
Hawakujiadaa kuongozwa na Rais Samia ndio maana Wamekuwa mbogo sio kwenye mkataba wa bandari tu bali kwenye utawala wa Rais Samia kwa ujumla.
Rejea mahojiano ya Slaa na star tv baada ya Rais samia kuapishwa, Slaa aliishambulia serikali na kuituhumu kuhusu kifo cha Rais Magufuli, Slaa akamalizia kwa kusema kama wanataka wanikamate,siogopi kukamatwa, alionekana ni mtu mwwnye hasira ya kukosa cheo.
Kwa msingi huo, huu ni uthibitisho kuwa Tamko lililoitwa la TEC lina msukumo wa kidini kuliko msukumo wa kisheria na kisiasa.
Nchi yetu ina dini kubwa Mbili, Wakristo na waislaam, tujaalie hilo ni tamko la wakatoliki.
Je na waislaam nao wakitoa tamko lao linalopingana na tamko la TEC?
Vipi walokole nao wakiunga mkono uwekezaji, serikali itafuata msimamo wa dini gani?
Ndio msingi uliosababisha serikali kutamka kuwa haina dini,lengo nikuepuka misuguano inayoweza kuliingiza taifa kwenye machafuko.
Tumeshatoa maoni,serikali imeyasikia na ndani ya serikali kuna watu wa dini zote na wasiokuwa na dini, kuna wanasheria kuna vyombo mbalimbali vya dola.
Ni imani yangu kuwa Swala la uwekezaji wa Bandari watalifanyia kazi kwa kulinda maslahi ya taifa.
Viongozi wa dini wasiingile utendaji wa serikali ambayo kila mmoja anatambua haina dini.
Tuwapuuze Slaa na kitima, wanataka kutuingiza kwwnye vita yao ya maslahi binafsi kwa Kisingizio cha kulinda rasilimali , tuulinde umoja wetu uliodumu kwa zaidi ya miaka 50.
Tujifunze Burundi na Rwanda, mauaji ya kimbali yalihamasishwa na viongozi wa dini.
Mpangawangu, kuna upotoshaji mkubwa kwenye huu uchambuzi wako:
1. Dr Padri Kitima, PhD ndiye mtendaji mkuu wa TEC. Hivyo kuandaa na kutoa hilo tamko la maaskofu wa TEC ni kati ya majukumu yake ya kazi. Kama ulitegemea litatolewa na mmojawapo wa hao maaskofu, utakuwa umekosea sana. TEC ina kanuni na taratibu zake za kiuendeshaji ambazo ni madhubuti.
2.1 Inaelekea hujui kazi na mamlaka ya Rais wa JMT. Ana kofia tatu: ni mkuu wa nchi, amiri mkuu wa majeshi yote ya JMT na ni mkuu wa serikali. Kwenye ukuu wa serikali ana saidiwa na makamu wa rais pamoja na waziri mkuu. Kwenye ukuu wa nchi na uamiri mkuu wa majeshi ni yeye peke yake, hakuna cha makamu, waziri mkuu wala msaidi ye yote kwenye mamlaka hayo.
2.2 Kwenye hiyo inayoitwa mihimili mitatu yaani bunge, mahakama na serikali, rais kwa moja ya kofia zake ndiye mkuu wa serikali akisaidiwa na baraza lake la mawaziri. Spika ndiye mkuu wa bunge anachaguliwa na wabunge wote (National Assembly).
Rais kwa kofia yake ya ukuu wa nchi ndiye humchagua mkuu wa mahakama ie Jaji Mkuu.
2.3 Kama mkuu wa nchi, Rais ana mamlaka ya mambo yote nchini kwake pamoja na hiyo mihimili yote ya nchi. Ana mamlaka ya kuvunja bunge lote akiona haliendeshwi vizuri kwa maslahi ya nchi, na kuitisha uchaguzi mkuu mpya. Ana mamlaka ya kumtengua mkuu wa mahakama na kumchagua mwingine akiona mahakama za nchi haziendeshwi vizuri kwa masilahi ya wananchi.
2.4 Kwa mamlaka haya makubwa ndiyo maana wananchi wote nchini huchagua mtu mmoja miongoni mwao wa kumkabidhi mamlaka hayo makubwa ayatekeleze kwa niaba yao. Uchaguzi huo hufanyika kwa kura za siri kwenye sanduku la kura wakati wa uchaguzi mkuu. Mkuu wa nchi ni mmoja tu, hii ndiyo principle ya utawala ambayo wahenga walisema, fahari wawili hawawezi kukaa zizi moja.
3. Umepotosha sana kulinganisha TICS na DP World. TICS hakuwa mmiliki wa bandari ya DSM. Ni kampuni kutoka Hong Kong iliyopewa kazi ya kupakua na kupakia makontena melini kwa ujira fulani toka serikalini kwa kipindi maalum na watanzania waliruhusiwa kununua shares kwenye kampuni hiyo. Wapo watanzania wengi tu walionunua shares hizo, mmojawapo ni huyo Karamagi aliyenunua shares za kutosha kuwa member wa Board of Directors wa kampuni hiyo.
TICS hawakuwa wamilki wa bandari ya DSM na wala hakukuwa na Intergovernmental Agreement kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya China kuhusu masharti ya ujio wa kampuni hii ya TICS. Hawa DP World ni tofauti kabisa. Ujio wao Tanzania utakuwa kwa mjibu wa masharti yaliyoko kwenye Intergovernmental Agreement kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Emirate ya Dubai. Masharti haya ni magumu sana na yanaipa kampuni ya DP World umiliki wa bandari zetu zote, maeneo maalum ya uchumi (special economic zones) na njia za usafirishaji. Umiliki huu kwa lugha ya kizungu ambacho akina Nape hawakifahamu unaitwa exclusive rights. Masharti hayo yayawapi ruhusa watanzania kununua shares kwenye kampuni hiyo, yayana kikomo cha muda wala hayana kiasi cho chote cha kitakakuwa kinalipwa serikalini.
4. Umepotosha kwamba Kitima hajawahi kumpinga Magufuli kwenye utawala wake. Kitima alimpinga kwa nguvu zote za namna Magufuri alivyokuwa kuficha takwimu za mlipuko wa ugonjwa wa uviko (covid 19) na kupuuzia masharti ya kukabiliana na gonjwa hilo yakiwemo yale ya lockdown na kuvaa barakoa. Kitima alitoa takwimu za mapadre 60 waliokufa kwa covid ndani ya mwezi mmoja. JPM alionesha kukerwa sana na matamko hayo ya TEC kupitia kwa Kitima. Ikumbukwe ni waziri wa afya, waziri mkuu au JPM mwenyewe ndiyo walikuwa mamlaka pekee ya kutangaza takwimu za wagonjwa wa covid. Kitima akaanza kuwa anatoa takwimu hizo. Jiwe lilimvumilia na kumpuuza.
5. Umepotosha kuhusu waarabu wenye mindevu mirefu waliokuwa wakijitokeza pale Kariakoo enzi za utawala wa Kikwete. Ukweli ni kuwa wakati huo ndio ambao Osama bin Laden alikuwa amefanya vitu vyako huko Amerika na kuwa tishio la dunia. Watu walipokuwa wakiona jitu linalofanana na Osama walikuwa wakiogopa sana na kukimbia ovyo. Hicho ndicho kilichokuwa kinafanyika hapo Kariakoo kwa nia ya kuwatisha na kuwaibia wafanyabiashara. Hicho ndicho Slaa alichokuwa akikemea, si uislamu.
6. Umepotosha chanzo cha urafiki wa Dr Slaa na Dr Magufuri. Ukweli ni kwamba kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015, huko chadema walivurugana kwa kumkata Dr Slaa na kumuingiza Edward Lowassa dakika za mwisho. Dr Slaa alichukia na kuanza kukipaka matope chama cha chadema, kunguru (ccm) walifurahi. Mbowe na cdm walichukia na kuanza kutishia maisha ya Slaa na ikabidi akimbilie Canada. Magufuli alifurahi na akampa ubalozi huko Sweden alikosomea hiyo PhD yake (Slaa) ili kuwauzi chadema. Huo ukawa urafiki wake na JPM.
Dr Slaa ana umri wa miaka 75 sasa, siyo zaidi ya 78 kama ulivyo andika. Hawapishani sana na Kinana. Ubalozi ni cheo cha kisiasa na hakina umri wa kustaafu. Hivyo Slaa hakustaafu kwa umri bali alistaafishwa (kutumbuliwa) na rais Salmia. Labda hili linaweza kumfanya akawa na kinyongo na rais Salmia.
7. Viongozi wa dini wana nafasi ya kipekee kwenye jamii. Tasisi za dini ni tasisi za jamii na husajiliwa huko BRELA kama tasisi za jamii. Masuluhisho ya kutoelewana ndani ya jamii mara nyingi hufanywa na viongozi wa dini au wazee maarufu aka wazee wa busara katika hiyo jamii. Hili la kutoelewana katika jamii ya watanzania kuhusu mkataba huu wa IGA ya bandari zetu, liko wazi. Jamii ya watanzania hawaelewani kwa zaidi ya miezi miwili sasa. Malumbano ni makali kila siku kila mahali: mitaani, majukwaani, mahakamani, redioni, kwenye tv, mitandaoni, magazetini, vyombo vya kimataifa nk. Jamii inatukanana na sasa kuna tishio la uvunjifu wa amani, polisi imebidi ianze kutumia ngvuvu na kuwasweka rumande wanaotishia amani. Ni muda mwafaka taasisi za dini na nyinginezo za ndani na nje kusuluhisha mzozo huu. Ni jukumu lake la kijamii.