Dkt. Charles Kitima na Dkt. Slaa wote wamewahi kuwa Makatibu wa TEC haya ndiyo maoni yangu kuhusu waraka wa TEC

Wakristo kwa unafki hawana mpinzani.

Kwenye udini huko ndo wamebobea cha ajabu wanawatupia zigo la udini waislamu.

Muhimu waislamu tunaelewa kinachoendelea.

Sisi tunaangalia tu mwisho wenu.

Angaikeni mnachokitengeneza na kukitafuta mtakipata.
Udini Tanzania utatumaliza. Mbona Kenya, Rwanda au Burundi tangu ipate uhuru haijawahi kutawaliwa na mwislam. Mmepewa shavu mnataka na kichwa?
 
Upo sahihi mkuu
 
Mpangawangu, kuna upotoshaji mkubwa kwenye huu uchambuzi wako:

1. Dr Padri Kitima, PhD ndiye mtendaji mkuu wa TEC. Hivyo kuandaa na kutoa hilo tamko la maaskofu wa TEC ni kati ya majukumu yake ya kazi. Kama ulitegemea litatolewa na mmojawapo wa hao maaskofu, utakuwa umekosea sana. TEC ina kanuni na taratibu zake za kiuendeshaji ambazo ni madhubuti.

2.1 Inaelekea hujui kazi na mamlaka ya Rais wa JMT. Ana kofia tatu: ni mkuu wa nchi, amiri mkuu wa majeshi yote ya JMT na ni mkuu wa serikali. Kwenye ukuu wa serikali ana saidiwa na makamu wa rais pamoja na waziri mkuu. Kwenye ukuu wa nchi na uamiri mkuu wa majeshi ni yeye peke yake, hakuna cha makamu, waziri mkuu wala msaidi ye yote kwenye mamlaka hayo.

2.2 Kwenye hiyo inayoitwa mihimili mitatu yaani bunge, mahakama na serikali, rais kwa moja ya kofia zake ndiye mkuu wa serikali akisaidiwa na baraza lake la mawaziri. Spika ndiye mkuu wa bunge anachaguliwa na wabunge wote (National Assembly).
Rais kwa kofia yake ya ukuu wa nchi ndiye humchagua mkuu wa mahakama ie Jaji Mkuu.

2.3 Kama mkuu wa nchi, Rais ana mamlaka ya mambo yote nchini kwake pamoja na hiyo mihimili yote ya nchi. Ana mamlaka ya kuvunja bunge lote akiona haliendeshwi vizuri kwa maslahi ya nchi, na kuitisha uchaguzi mkuu mpya. Ana mamlaka ya kumtengua mkuu wa mahakama na kumchagua mwingine akiona mahakama za nchi haziendeshwi vizuri kwa masilahi ya wananchi.

2.4 Kwa mamlaka haya makubwa ndiyo maana wananchi wote nchini huchagua mtu mmoja miongoni mwao wa kumkabidhi mamlaka hayo makubwa ayatekeleze kwa niaba yao. Uchaguzi huo hufanyika kwa kura za siri kwenye sanduku la kura wakati wa uchaguzi mkuu. Mkuu wa nchi ni mmoja tu, hii ndiyo principle ya utawala ambayo wahenga walisema, fahari wawili hawawezi kukaa zizi moja.

3. Umepotosha sana kulinganisha TICS na DP World. TICS hakuwa mmiliki wa bandari ya DSM. Ni kampuni kutoka Hong Kong iliyopewa kazi ya kupakua na kupakia makontena melini kwa ujira fulani toka serikalini kwa kipindi maalum na watanzania waliruhusiwa kununua shares kwenye kampuni hiyo. Wapo watanzania wengi tu walionunua shares hizo, mmojawapo ni huyo Karamagi aliyenunua shares za kutosha kuwa member wa Board of Directors wa kampuni hiyo.

TICS hawakuwa wamilki wa bandari ya DSM na wala hakukuwa na Intergovernmental Agreement kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya China kuhusu masharti ya ujio wa kampuni hii ya TICS. Hawa DP World ni tofauti kabisa. Ujio wao Tanzania utakuwa kwa mjibu wa masharti yaliyoko kwenye Intergovernmental Agreement kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Emirate ya Dubai. Masharti haya ni magumu sana na yanaipa kampuni ya DP World umiliki wa bandari zetu zote, maeneo maalum ya uchumi (special economic zones) na njia za usafirishaji. Umiliki huu kwa lugha ya kizungu ambacho akina Nape hawakifahamu unaitwa exclusive rights. Masharti hayo yayawapi ruhusa watanzania kununua shares kwenye kampuni hiyo, yayana kikomo cha muda wala hayana kiasi cho chote cha kitakakuwa kinalipwa serikalini.

4. Umepotosha kwamba Kitima hajawahi kumpinga Magufuli kwenye utawala wake. Kitima alimpinga kwa nguvu zote za namna Magufuri alivyokuwa kuficha takwimu za mlipuko wa ugonjwa wa uviko (covid 19) na kupuuzia masharti ya kukabiliana na gonjwa hilo yakiwemo yale ya lockdown na kuvaa barakoa. Kitima alitoa takwimu za mapadre 60 waliokufa kwa covid ndani ya mwezi mmoja. JPM alionesha kukerwa sana na matamko hayo ya TEC kupitia kwa Kitima. Ikumbukwe ni waziri wa afya, waziri mkuu au JPM mwenyewe ndiyo walikuwa mamlaka pekee ya kutangaza takwimu za wagonjwa wa covid. Kitima akaanza kuwa anatoa takwimu hizo. Jiwe lilimvumilia na kumpuuza.

5. Umepotosha kuhusu waarabu wenye mindevu mirefu waliokuwa wakijitokeza pale Kariakoo enzi za utawala wa Kikwete. Ukweli ni kuwa wakati huo ndio ambao Osama bin Laden alikuwa amefanya vitu vyako huko Amerika na kuwa tishio la dunia. Watu walipokuwa wakiona jitu linalofanana na Osama walikuwa wakiogopa sana na kukimbia ovyo. Hicho ndicho kilichokuwa kinafanyika hapo Kariakoo kwa nia ya kuwatisha na kuwaibia wafanyabiashara. Hicho ndicho Slaa alichokuwa akikemea, si uislamu.

6. Umepotosha chanzo cha urafiki wa Dr Slaa na Dr Magufuri. Ukweli ni kwamba kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015, huko chadema walivurugana kwa kumkata Dr Slaa na kumuingiza Edward Lowassa dakika za mwisho. Dr Slaa alichukia na kuanza kukipaka matope chama cha chadema, kunguru (ccm) walifurahi. Mbowe na cdm walichukia na kuanza kutishia maisha ya Slaa na ikabidi akimbilie Canada. Magufuli alifurahi na akampa ubalozi huko Sweden alikosomea hiyo PhD yake (Slaa) ili kuwauzi chadema. Huo ukawa urafiki wake na JPM.
Dr Slaa ana umri wa miaka 75 sasa, siyo zaidi ya 78 kama ulivyo andika. Hawapishani sana na Kinana. Ubalozi ni cheo cha kisiasa na hakina umri wa kustaafu. Hivyo Slaa hakustaafu kwa umri bali alistaafishwa (kutumbuliwa) na rais Salmia. Labda hili linaweza kumfanya akawa na kinyongo na rais Salmia.

7. Viongozi wa dini wana nafasi ya kipekee kwenye jamii. Tasisi za dini ni tasisi za jamii na husajiliwa huko BRELA kama tasisi za jamii. Masuluhisho ya kutoelewana ndani ya jamii mara nyingi hufanywa na viongozi wa dini au wazee maarufu aka wazee wa busara katika hiyo jamii. Hili la kutoelewana katika jamii ya watanzania kuhusu mkataba huu wa IGA ya bandari zetu, liko wazi. Jamii ya watanzania hawaelewani kwa zaidi ya miezi miwili sasa. Malumbano ni makali kila siku kila mahali: mitaani, majukwaani, mahakamani, redioni, kwenye tv, mitandaoni, magazetini, vyombo vya kimataifa nk. Jamii inatukanana na sasa kuna tishio la uvunjifu wa amani, polisi imebidi ianze kutumia ngvuvu na kuwasweka rumande wanaotishia amani. Ni muda mwafaka taasisi za dini na nyinginezo za ndani na nje kusuluhisha mzozo huu. Ni jukumu lake la kijamii.
 
Nivema
Ukaifahamu Kwanzaa TEC na muundo wake

Ukiona katibu mkuu wao anasema jambo,anawasilisha maazimio ya maaskofu sio anatoa kichwani kwake yeye....
 
Udini Tanzania utatumaliza. Mbona Kenya, Rwanda au Burundi tangu ipate uhuru haijawahi kutawaliwa na mwislam. Mmepewa shavu mnataka na kichwa?
Kwani nyie ndo wamiliki wa Tanzania?
 
MKuu
Umemjadili Kitima.

Tujadili contents za TAMKO la TEC

Unalazimisha udini pasipostahili
Unaandika madude mengi hayana maana kwahiyo Ma Askofu wote wangejazana kwenye chumba cha Habari
 
Tuwapuuze Slaa na kitima, Slaa ni mchumia tumbo tu.
 
Kumbe bado mnawafikiria TEC
Si mmesema nyingi kuwa kwani TEC ni akina nani hii nchi na Wana mchango gani serikalini

Kumbe wanawawazisha!
 
Povu kama lote.

Wangetoa tamko la kuunga mkono sijui kama ungekuja na taulo mkononi kama hivi
Mi mwenyewe siungi mkono mkataba, ila taasisi za kidini hazitakiwi kutoa matamko yao, wawaache waumini na misimamo yao.
 
MKuu
Umemjadili Kitima.

Tujadili contents za TAMKO la TEC

Unalazimisha udini pasipostahili
@mgangawangu post kama unatakiwa kuzitafakari kabla ya kuleta pumba zako JF. Hutaki kabisa kujadili maudhui ya waraka wa TEC wala contents za IGA?! Seriously?
 
Dah bonge Moja la Uzi pig up mkuu umetiririka vyema sana
 
una akili sana hii reasoning inayotakiwa. wengine akiongea askofu baasi wanaaacha kufikiria
Wanaamini hao akisema askofu ukimpinga umepingana na Mungu sisi hatuko hivyo wasituletee misingi Yao ya kikatoliki nchi hii haiongozwi kikatoliki
 
Hebu tuwekee hapa ushahidi kuwa Pd. Kitima ana maslahi binafsi hapo bandarini. Ila wakati mwingine jitahidi kupinga hoja na sio kumshambulia mtoa hoja.
 
Mi mwenyewe siungi mkono mkataba, ila taasisi za kidini hazitakiwi kutoa matamko yao, wawaache waumini na misimamo yao.
Viongozi wa Taasisi za dini hawana haki juu ya nchi Yao? Wasiposema wao nani atasema? Yule shehe wa Dar es Salaam anayetoaga onyo na tahadhari kwa wanaokosoa mambo ya DPw anapata wapi uhalali ule?! Tusidanganyane katika kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…