DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Mhadhiri wa sayansi ya siasa wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Dk Conrad Masabo anasema demokrasia ya Tanzania iliharibiwa tangu mwaka 2016 kutokana na uamuzi uliofanywa na Watanzania kuamini mtu na sio utaratibu.
“Tunachokipitia ni matokeo ya huo uamuzi wetu. Demokrasia kama haki nyingine hudaiwa na sio kuombwa, pia inapaswa kulindwa ili walioitoa wasiipokonye tena,” anasema.
Katika kipindi hicho, Dk Masabo anasema Watanzania wote waliamini Hayati John Magufuli ni mkombozi na 2021 waliamini Rais Samia Suluhu Hassan atawakomboa, hadi kupigiwa chapuo na vyama vya upinzani.
Kwa mtazamo wa mwanazuoni huyo, kwa hali ilivyo hadhani kama maboresho yanawezekana.
Hata hivyo, anaeleza uwezekano upo katika mambo mawili ambayo ni kuja kwa kiongozi mwenye hisani aijenge demokrasia licha ya kuwa jambo hilo ni gumu kwa mfumo wa demokrasia ya vyama uliopo.
Jambo la pili, anasema wananchi wajiunge kuidai, kitu ambacho ni kigumu kwa vile raia wameamua kuwaachia wanasiasa jukumu hilo.
“Kuna uwezekano mkubwa wa kulipa thamani kubwa ili kurejea tulipokuwa mwaka 2015, swali ni nani wa kulipa gharama hii?” anahoji.
Dk Masabo anasema kinachoitesa Tanzania ni kwa sababu demokrasia yake ni ya vyama na sio ya raia, hivyo raia au wananchi wanaamini hawana wajibu wa kudai na kuilinda.
“Mafanikio ya Reject Financial Bill (kuondolewa kwa muswada wa fedha) ya Kenya ni kwa vile ilikuwa inaongozwa na kusimamiwa na raia na ndio maana baada ya vyama kuingia, malengo na mafanikio yamepotea,” anafafanua.
Credit: JamboTv