Dkt. Dorothy Gwajima: Kama unataka nitumbuliwe ili uchukue nafasi yangu, fanya kazi zaidi yangu sio ufitini

Pole Dr Gwajima, hapo ndipo Watanzania tunapofeli, siyo ajabu wawekezaji toka nje kupendelea kuajiri watu wao, manyang'au na watu toka nje ya nchi, yaani sisi ni wavivu, fitina na majungu tu! Vyeti vyenyewe vya kubabaisha, kazi ipo kwa kweli..
 
Hizo dawa zilikuwa upende wa bima ambapo kimsingi ni pharmacy inayojitegemea kwa ajili ya watu wa bima na cash pekee. Ukiwekee hizo dawa Kwenye dirisha la kawaida vidonge 3000 havimaliiz hata siku moja .pcm ni dawa inayotumika kwa wengi sana hasa Kwenye makundi ya msamaha Kama wazee watoto na wajawazito
 
Kwani sera na mifumo ya kufikisha dawa kwa mlaji hazipo? Tatizo siyo sera na mifumo, tatizo ni kwamba nyie ni WEZI. Badilikeni muache wizi muone kama dawa hazitamfikia mlaji!
.....
 

Attachments

  • sp_agahtkc_s1610043012.png
    65.1 KB · Views: 1
Huyu mama ni punguani sana siku hizi anavaa mgole wa bendera begani akijinadi ni mfia nchi. Anadhalilisha sana watu huyu mama. Kwanini asiwe na vikao nao vya ndani kabla ya kuanza upupu wake. Atulize bori 84% winner hapendi ujinga atamshangaza.
Tunasema hivi..mlizoea kuchukua madawa na kuhamishia madukani mwenu,kutibu wagonjwa kwa kitu kidogo,kwenda kunywa chai ilihali wagonjwa wanaugulia maumivu kwenye benchi..ngoja mkome
 
Huduma mbaya kwa kiasi kikubwa inatokana na serikali yenyewe japo kuna mapingufu kwa baadhi ya watumishi lakini haiondoi ukweli Kuwa serikali haitaki kuwekeza huko ila nataka mtumishi ndo abebe lawa zote. Mfano serikali inasema wazee waja wazito na under 5 wote watibiwe bure sasa hela ya kuwatibu bure hawalete na mama na wazee wanaaminihwa hivyo Kuwa watatibiwa bure .sasa akija akikuta baadhi ya dawa hamna ndo hapo naona huduma mbovu
 
Mtaweza kweli kufanya kazi NHS; ngoja nikupe mfano wenzetu wanavyofanya mambo mgonjwa akiingia na hyperglycaemia, loss of appetite na dehydration ata kama dawa zake kabla zilikuwa ni kwenye ku boost insulin tu na tatizo lenyewe la awali lilikuwa bado lipo kwenye mmol/mol za kawaida za diabetes . Anaporudi na hyperglycaemia kabla ujajua sababu za ongezeko la sukari na ukubwa wa ongezeko; role ya mgonjwa kwenye ongezeko iwe uzembe wake wa kutumia dawa au kuna issue za gastroparesis kitu unachotakiwa kufikiria wakati vipimo avijarudi ni kuzuia madhara ambayo ujayaona.

Sasa boss wako aje akute mgonjwa hana fluid za kumlinda dhidi ya risk za acute deceleration kutokana na madhara mengine ya ugonjwa wake kwa madai ya kwamba aitaji kwa sababu hakuna huo ushahidi. Na sababu zako kuna wagonjwa million 3 wengine wenye HHS watahitaji zaidi tazocin na Hartman’s; wewe kama ni repeated offender usiefuata admission note aliyokuachia mwenzako to minimise the risk associated with the patient long term condition unaweza jikuta unachukuliwa disciplinary action.

Dr kaandika mgonjwa apewe paracetamol (atujui na dawa zingine kutokana na ugonjwa wenyewe) sio shughuli ya pharmacy kusema nani apate nani akose, ni hivi wamekosea na wajifunze mpaka watu wakashitaki kwa mkuu wa wilaya ina maana wanahitaji hizo paracetamol.

God knows watu wangapi wanakufa kwa uzembe kama huu wa watu kama nyie kujifanya wajuaji stick to the rules sio kutaka kujifanya wabunifu na maisha ya watu.

Hizi ndio sababu unakuta watu wenye long term medical conditions unasikia aliumwa ghafla akaenda hospitali akapata nafuu aliporudu siku chache akazidiwa akafa: ni uzembe wa hospitali kutochukua precautionary measures given the patient condition before the test results; worst vipimo vyenyewe Dr Gwajima katuonyesha wana tabia ya kuchelewa maabara. No wonder mnamlilia Ummy Mwalimu.

The bottom line wamekosea hao jamaa huko juu kama wana akili timamu Dr Gwajima wanatakiwa wamuwekee ring fence na haya majungu she knows her stuff sio watu tia maji tia maji wanaotetea upuuzi kesho si mtaambiwa mtu mumpe dawa serious mtasema anaonekana ahitaji wewe ndio daktari uliemuandikia prescription.

Someone needs to sort that mess na hii culture ya baadhi ya madokta wetu kujifanya wajuaji sana, mtu anatakiwa apeleke damu ikapimwe ndani ya siku 10; zinapita kuna mlundikano wa damu mpaka bank inajaa halafu kuna wapuuzi wanatetea.

Anachofanya Dr ni ku expose nonsense za wizara ya afya na wengine wapate habari jirekebisheni. Sio kutetea ujinga ujinga.
 
Mtanzania yeyote mwenye akili timamu akipitia chapisho lako atajua tu kwamba wewe ni member wa genge lililo jipanga kumwaribia sifa Dk. Gwajima - na wewe unaonekana si mbumbumbu hupo kwenye fani hii hii ya kitabibu.

Kwa kuwa Dk.Gwajima kawashika pabaya ndio maana mmejipanga kubumba shutuma za kishenzi ili Gwajima aonekane hafahi, mnacho sahau ni kwamba Dk.Magufuli haku bahatisha katika teuzi zake za kumkabidhi Dk.Gwajima ili asimamie Wizara hii ambayo ni pasua kichwa - baadhi ya madaktari/famasia hawana uzalendo hata kidogo wameigeuza/run Wizara ya afya kama mali ya ukoo - wizi wa madawa ambayo Serikali inatumia fedha nyingi za kigeni kuziagiza kutoka nje ya Nchi, mwisho wa siku zanaishia kwenye maduka ya madawa yanayo milikiwa na baadhi ya madaktari na wafamasia.

Ni wazi Dk.Gwajima knows Wizara ya afya like back of her hand, umudanganyi kitu - sasa watu wezi kama nyinyi hamuwezi kumpenda/kuwa na ushirikiano wa karibu ni mtu kama Dk.Gwajima mtampiga vita tu mkitegemea kwamba Dk.Magufuli atawekea maanani uzushi wenu wa kijinga ili mwisho wa siku JPM atamtumbue Dk.Gwajima muwe free kuendeleza hujuma zenu pakiwemo na wizi wa madawa.
 
Aliyemwambia kuwa watu wanaitaka nafas yake ni nani?

Ye afanye kazi kistaarabu, aache kudhalilisha watumishi wake...


Ila nadhan "ndoa" yake ina walakini...ama kuna shida kichwani hayuko sawa
Wajumbe kama mumehisi ana kichaa bac ni moja kati ya category muhimu ya mkuu wa Maya yetu hii TZ
 
Mwacheni afanye kazi, anakosoa na kutoa udhaifu unaotokea "amefuta maiti kudaiwa bill", amefuta mazoea ya kila mtendaji wa wizara kuamka na kwenda mkoani eti kufanya ufuatiliaji na badala yake waorodheshe shughuli muhimu na kwenda kama timu ili kuokoa fedha",

Sasa hapo ana kosa gani "kujiita field marshal" si dhambi na actually kwa sasa ktk sekta hiyo as long as ni waziri yes ni Field Marshal ktk Wizara yake.
 
Kuna watu wengine hawapaswi kua viongozi , walaitakiwa waendelee kua watenadaji wakawaida serekalini
 
Yupo mshikaji mmoja familia yake inaishi UK yeye muda mwingi yupo Tanzania miaka kama mitatu nyuma familia wamekuja holiday ana binti wa 11 ni mdhaifu kiafya (nimesahau maradhi yake halisi).

Baada ya week mtoto kaanza kuumwa taratibu wamempleka hospitali jamaa awajachukua vipimo vyote wanamwambia sio serious as far as mama mtu is concerned maneno ya daktari yana halalisha kuendelea na bata lake.

Baba mtu japo anaishi Tanzania na yeye ana makaratasi ya kuingia huko kila akimwangalie mwanae anaona hapana huyu mtoto anaumwa mama mtu kurudi na mtoto ataki hospitali washasema sio serious yeye lazima amalize week sita zake za likizo.

Jamaa akaona isiwe kesi akaacha shughuli zake akakata ticket ya haraka huyo UK anakwambia ile kufika Gatwick hali ikabadalika ghafla wazungu walipomuona mtoto hapo hapo ikaitwa ambulance akapelekwa hospitali kufika hospitali moja kwa moja intensive care; madokta wanamwambia ulifanya la maana kumuwaisha without serious medical intervention alikuwa anaondoka.

Ndio aina ya madaktari kama huyu Zithromax yeye hajui kwanini mtu kaambiwa atumie dawa fulani anakuja hapa kutuambia hao wanaonyimwa awazihitaji hii culture ya wataalamu wetu ni shida.
 
Ulinzi sio nyeti mzee labda mambo ya ndani, Waziri wa Ulinzi ni Ceremonial figure
Muwe waelewa unaposema Wizara haumaanishi mtu una maanisha mambo ambayo yanafanywa na wizara hiyo yaa majukumu ya Wizara, sasa ukisema ulinzi siyo nyeti napata mashaka na uwezo wako wa kupambanua mambo kwa usahihi.
 
Mkuu unakwama wapi hayo maelezo mbona hata hayahusiana na hii topic .katika setting za kawaida kuna dirisha la bima na cash hili linajiendesha Kama private japo unakuwa chini ya Moi na maelezo ya kufungua haya maduka aliyatoa Huyu waziri akiwa huko tamisemi na mara nyingi linajiendesha lenyewe biala shida na hapa sio rahis kukosa dawa kwa Kuwa ni either kulipia au NHif dirisha la piling ni la kawaida maana huko ndo wagonjwa wa msamaha wale wazee wanarundikana huko na dawa zao huwa hazikatikiz Zikija
 
hapo hao jamaa wasingeweza kuchomoka, maana huo ni udanganyifu mkubwa. kuna sehemu alikuja nikaona wanahangaika kutafuta dawa ili ikitokea amefika zionekane. mi nikasema shida hizi zote za nini si bora tu mseme ukweli hamna ili msaidiwe.
 
hapo hao jamaa wasingeweza kuchomoka, maana huo ni udanganyifu mkubwa. kuna sehemu alikuja nikaona wanahangaika kutafuta dawa ili ikitokea amefika zionekane. mi nikasema shida hizi zote za nini si bora tu mseme ukweli hamna ili msaidiwe.
Hiyo kesi yenyewe ya paracetamol kapewa na mkuu wa wilaya yeye alikuwa kaenda kukagua hospitali kama inafaa kupandishwa hadhi.

Mkuu wa wilaya baada ya kupokea malalamiko alikuwa akienda kuulizia wanamwambia hakuna; na yeye wakataka kumchukulia poa ndio akaanza kazi ndani ya muda mchache wa auditing ikabidi waseme ukweli wanazo.

Tena hiyo ilikuwa haraka ndio akawauliza hapa sasa ikifanyika full audit si itakuwa tatizo ndio maana akawaita waongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…