DOKEZO Dkt. Dorothy Gwajima tupia macho chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama, kuna madudu mengi na mtiririko wa elimu usioeleweka katika mifumo ya Serikali

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwanza, ninaomba kutangaza "Conflict of Interest" katika jambo hili. Ninaandika haya baada ya kuwa mimi ni sehemu ya waathirika wa mfumo wa elimu unaotolewa na Chuo cha Ustawi wa Jamii.

Nilikuwa nina watoto watatu ambao nimekuwa nikiwasaidia kupata elimu hapo. Hawa ni watoto wa washirika na jamaa zangu waliotangulia mbele za haki. Ninapoangalia makaburi yao, marumaru, na nukuu za Biblia zilizoandikwa katika kuta za makaburi hayo, ninakumbuka ujana wetu wa pamoja na hisia za ujamaa. Ninaona deni langu kwao kutokana na maisha tuliyoishi.

Kwa kufuata ushauri wa wataalamu, nilipeleka watoto kusoma katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama, ambacho kipo chini ya Wizara ya mdogo wangu, Dkt. Gwajima D .

Mmoja alijikita katika shahada ya kwanza ya Mahusiano Kazini na Utawala wa Umma, ambayo awali ilikuwa ikijulikana kama "Industrial Relations". Mwingine alisoma elimu ya awali (Chekechea) na baadaye cheti cha ustawi wa jamii. Kwa bahati mbaya, mmoja wao alilazimika kuacha masomo na sasa yupo VETA akijifunza kupaka rangi.

Bahati mbaya, mwenye shahada ya "Labour Relations and Public Management" ameshindwa kupata ajira rasmi serikalini kwa sababu shahada hiyo haitambuliki katika "Scheme of Service". Licha ya serikali kumiliki Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama na kutoa mikopo na idhibati ya elimu, mifumo yake haiitambui shahada hiyo. Hii inawafanya wahitimu wasiajirike serikalini.

Kwa Mama Gwajima, kama msimamizi wa wizara husika, na kwa Waziri wa Elimu, naomba mshughulikie suala hili kwa pamoja ili kuwasaidia vijana hawa. Kwa nini serikali moja inakuwa na lugha gongana? Ninaandika kama mmoja wa waathirika wa mfumo huu.

Masikitiko yangu kwa chuo hiki pia ni mashaka ya ubora wa elimu. Mmoja wa watoto alikosa sifa za kuendelea na chuo kwa sababu GPA yake ilikuwa chini ya 2.0. Nilijiandaa kumpeleka VETA, lakini alinijulisha kuwa chuoni kwao, usipofikisha GPA unapewa mtihani maalumu ili ku-boost GPA na unaendelea na masomo. Je, huu ni utaratibu unaoruhusiwa?

Idara ya elimu inaonekana kuwa na matatizo. Wanafunzi wanadekezwa na management, na wakuu wa idara wanaogopa kujibu maswali kuhusu GPA ndogo na kufeli. Hii ni hatari kwa mustakabali wa elimu ya watoto na taifa kwa ujumla.

Ninaamini Waziri mwenye dhamana anapaswa kuangalia chuo hiki, kuanzia utawala hadi ofisi za wanataaluma, ili kuboresha ubora wa elimu na uhusiano kati ya kozi zinazotolewa na mfumo wa ajira wa serikali.

Ninayaandika haya kwa ajili ya wazazi wengine ambao wanapanga kupeleka watoto wao katika chuo hiki. Wajue kuwa kuna changamoto ambazo tumezipitia.

Ni matumaini yangu, Waziri husika atalifanyia kazi jambo hili.
Haya Ungepokea chuoni na pia kwa km wa wizara

Tusipoangalia kuna siku tutamtuma Dr Gwajima kutununulia fegi
 
Nipo na tumshukuru Mungu kwa kutupa uzima na afya.Nipo nimerudi tena ndugu
Nilipoona barafu na hiyo tarehe ya uzi, nikashukuru Mungu kwa kuona upo hai ndugu.
Ulipotea sana hapa jukwaani.

Kuhusu hilo la Ustawi naamini kwa dada yetu Dkt. Gwajima D atalifanyui kazi maana yupo humu na ni mfuatiliaji mzuri sana.
 
Haya Ungepokea chuoni na pia kwa km wa wizara

Tusipoangalia kuna siku tutamtuma Dr Gwajima kutununulia fegi

Unahoja lakini ameona bora ailete hapa kwa heshima ya JF ili na wengine watoe maoni yao.

Kubwa zaidi, kama alivyoeleza barafu , hiki chuo kipo chini ya wizara ya ustawi wa jamii na kwa sasa, waziri wake tunae hapa tena ni mchangiaji mzuri tu. Nna Imani taarifa itamfikia na kuchukua hatua stahiki.

Pia kuna wadau wengine wanaoweza kuchukua maamuzi kwenye kurekebisha hii hali na kuboresha wako hapa hapa JF hata kama hawatumii majina yao halisi.

Hajakurupuka na kamwe haitatokea Barafu atume waziri fegi.
 
Unahoja lakini amepona Bora ailete hapa Kwa heshima ya JF ili na wengine watoe maoni yao.

Kubwa zaidi, kama alivyoeleza barafu , hiki chuo kipo chini ya wizara ya ustawi wa jamii na Kwa Sasa, waziri wake tunae hapa tena ni mchangiaji mzuri tu. Nna Imani taarifa itamfikia na kuchukua hatua stahiki.

Pia kuna wadau wengine wanaoweza kuchukua maamuzi kwenye kurekebisha hii Hali na kuboresha wako hapa hapa JF hata kama hawatumii majina Yao halisi.

Hajakurupuka na kamwe haitatokea Barafu atume waziri fegi.
Asante sana kwa mchango wako
 
Kwanza, ninaomba kutangaza "Conflict of Interest" katika jambo hili. Ninaandika haya baada ya kuwa mimi ni sehemu ya waathirika wa mfumo wa elimu unaotolewa na Chuo cha Ustawi wa Jamii.

Nilikuwa nina watoto watatu ambao nimekuwa nikiwasaidia kupata elimu hapo. Hawa ni watoto wa washirika na jamaa zangu waliotangulia mbele za haki. Ninapoangalia makaburi yao, marumaru, na nukuu za Biblia zilizoandikwa katika kuta za makaburi hayo, ninakumbuka ujana wetu wa pamoja na hisia za ujamaa. Ninaona deni langu kwao kutokana na maisha tuliyoishi.

Kwa kufuata ushauri wa wataalamu, nilipeleka watoto kusoma katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama, ambacho kipo chini ya Wizara ya mdogo wangu, Dkt. Gwajima D .

Mmoja alijikita katika shahada ya kwanza ya Mahusiano Kazini na Utawala wa Umma, ambayo awali ilikuwa ikijulikana kama "Industrial Relations". Mwingine alisoma elimu ya awali (Chekechea) na baadaye cheti cha ustawi wa jamii. Kwa bahati mbaya, mmoja wao alilazimika kuacha masomo na sasa yupo VETA akijifunza kupaka rangi.

Bahati mbaya, mwenye shahada ya "Labour Relations and Public Management" ameshindwa kupata ajira rasmi serikalini kwa sababu shahada hiyo haitambuliki katika "Scheme of Service". Licha ya serikali kumiliki Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama na kutoa mikopo na idhibati ya elimu, mifumo yake haiitambui shahada hiyo. Hii inawafanya wahitimu wasiajirike serikalini.

Kwa Mama Gwajima, kama msimamizi wa wizara husika, na kwa Waziri wa Elimu, naomba mshughulikie suala hili kwa pamoja ili kuwasaidia vijana hawa. Kwa nini serikali moja inakuwa na lugha gongana? Ninaandika kama mmoja wa waathirika wa mfumo huu.

Masikitiko yangu kwa chuo hiki pia ni mashaka ya ubora wa elimu. Mmoja wa watoto alikosa sifa za kuendelea na chuo kwa sababu GPA yake ilikuwa chini ya 2.0. Nilijiandaa kumpeleka VETA, lakini alinijulisha kuwa chuoni kwao, usipofikisha GPA unapewa mtihani maalumu ili ku-boost GPA na unaendelea na masomo. Je, huu ni utaratibu unaoruhusiwa?

Idara ya elimu inaonekana kuwa na matatizo. Wanafunzi wanadekezwa na management, na wakuu wa idara wanaogopa kujibu maswali kuhusu GPA ndogo na kufeli. Hii ni hatari kwa mustakabali wa elimu ya watoto na taifa kwa ujumla.

Ninaamini Waziri mwenye dhamana anapaswa kuangalia chuo hiki, kuanzia utawala hadi ofisi za wanataaluma, ili kuboresha ubora wa elimu na uhusiano kati ya kozi zinazotolewa na mfumo wa ajira wa serikali.

Ninayaandika haya kwa ajili ya wazazi wengine ambao wanapanga kupeleka watoto wao katika chuo hiki. Wajue kuwa kuna changamoto ambazo tumezipitia.

Ni matumaini yangu, Waziri husika atalifanyia kazi jambo hili.
Habari za masiku mtaalam wa ndege
 
Back
Top Bottom