Dkt. Doto Biteko: Bwawa la Mwalimu Nyerere lina uwezo wa kuilisha Nchi hii umeme peke yake

Dkt. Doto Biteko: Bwawa la Mwalimu Nyerere lina uwezo wa kuilisha Nchi hii umeme peke yake

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Mashine ya tisa ya mtambo wa kuzalisha umeme katika Bwawa la Julius Nyerere Machi 22, 2025 imekabidhiwa na kuunganishwa kwenye Grid ya Taifa. Amesisitiza kuwa kutokana na ongezeko hilo la megawati za umeme Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere pekee linaweza kutosheleza mahitaji ya nchi licha ya kumalizika kwa muda uzalishaji wa umeme kwa kutumia mitambo ya Songas.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Machi 23, 2025 jijini Arusha wakati akitoa takwimu kuhusu ongezeko la mahitaji ya umeme nchini katika Kikao cha Baraza Kuu la Wazazi Taifa.

Pia soma: TANESCO, zipi faida za kuwa na bwawa kubwa la Umeme la Julius Nyerere (JHPP) ikiwa Unit 1 ya Umeme wateja wa T1 tunatozwa Sh 292?
 
Songas alikuwa mjanja mjanja wa umeme wa gesi

Mwarabu apigiwe makofi kwa kumaliza kazi kubwa
 
Back
Top Bottom