Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Mashine ya tisa ya mtambo wa kuzalisha umeme katika Bwawa la Julius Nyerere Machi 22, 2025 imekabidhiwa na kuunganishwa kwenye Grid ya Taifa. Amesisitiza kuwa kutokana na ongezeko hilo la megawati za umeme Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere pekee linaweza kutosheleza mahitaji ya nchi licha ya kumalizika kwa muda uzalishaji wa umeme kwa kutumia mitambo ya Songas.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Machi 23, 2025 jijini Arusha wakati akitoa takwimu kuhusu ongezeko la mahitaji ya umeme nchini katika Kikao cha Baraza Kuu la Wazazi Taifa.