BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania (AG), Dk Eliezer Feleshi amewataka mawakili wa Serikali kujitathimini kama wanaendana na dhima na kujitosheleza kwa nafasi walizopewa. Dk Felishi amesema hayo leo Jumatano, Septemba 28, 2022 wakati akifungua mkutano wa mawakili wa Serikali ulioandaliwa na ofisi yake.
“Jitathimini mwenyewe, kuna wagumu wa kujitathimini kwa sababu ni mabwana wasio na makosa, basi waambie wengine wakutathimini. Huwezi wewe kujitathimini weka mifumo ya wewe kupata mrejesho,” amesema.
Amesema kwa kuweka mifumo ya kujitathimini kiongozi atajua udhaifu wake upo wapi na kuchukua hatua ili aweze kwenda mbele. Pia, amewataka viongozi hao kuweka mikakati ya kujengeana uwezo kwa warsha, kuwasimamia, semina na mikutano.
“Kuna watu wa ajabu kabisa Mungu amekujalia umesoma, halafu hutaki wenzako waendelee, ni sawa na ibilisi kabisa. Kwasababu siku ya mwisho Mungu atakuhoji wangapi ulichangia wakaelewa kazi,” amesema.