Lakini kwa upande wa pili, Masauni naye anataka aonekane anao umwamba wa kuwatia jamba jamba CHADEMA. Tatizo ni wapi inapoishia serikali na wapi kinapo anzia chama; maana watu ni wale wale toka CCM.
..juzi tulikuwa tunaambiwa Chadema nzima ni Ccm.
..Sasa sijui imekuwaje wamewatumia Polisi kuwabamiza.
..yaani ni sawa na mtu awe na kimada halafu amtumie wahuni kumpiga au kumkaba. Juu ya nini?
..nadhani wanaoogopwa ni VIJANA / KIZAZI CHA SEKONDARI ZA KATA.
..Hawa vijana wakichangamana na Chadema kwa muda wa kutosha, CCM wanaweza kuingia matatani.
..Kwa hiyo, CCM sasa hivi haitaki Chadema iwekeze kwa wananchi, na haswa hilo kundi la vijana. Na hiyo ni kwasababu CCM haijawekeza kwenye mahitaji, na changamoto, za kundi hilo.