Pre GE2025 Dkt. Emmanuel Nchimbi kauli yako ya kuwaachia viongozi wa CHADEMA imekaa kimaigizo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lakini kwa upande wa pili, Masauni naye anataka aonekane anao umwamba wa kuwatia jamba jamba CHADEMA. Tatizo ni wapi inapoishia serikali na wapi kinapo anzia chama; maana watu ni wale wale toka CCM.

..juzi tulikuwa tunaambiwa Chadema nzima ni Ccm.

..Sasa sijui imekuwaje wamewatumia Polisi kuwabamiza.

..yaani ni sawa na mtu awe na kimada halafu amtumie wahuni kumpiga au kumkaba. Juu ya nini?

..nadhani wanaoogopwa ni VIJANA / KIZAZI CHA SEKONDARI ZA KATA.

..Hawa vijana wakichangamana na Chadema kwa muda wa kutosha, CCM wanaweza kuingia matatani.

..Kwa hiyo, CCM sasa hivi haitaki Chadema iwekeze kwa wananchi, na haswa hilo kundi la vijana. Na hiyo ni kwasababu CCM haijawekeza kwenye mahitaji, na changamoto, za kundi hilo.
 
Nawe unaamini kukamatwa Kwa viongozi CHADEMA, CCM haikuhusika Kutoa maelekezo?

Au tuamini kuwa upo mgawanyiko ndani ya chama?
Umeuliza maswali mazuri, ambayo nilisha anza kujiuliza nilipo fungua mada hii..

Masauni ndiyo anaye shikilia jeshi la polisi sasa hivi, na kaonyesha wazi yupo tayari kutumia kifaa hicho kumrudisha madarakani 'Chura Kiziwi'.
Kwa hiyo Masauni ana 'assignment' maalum, ambayo hata mama anaijuwa. Masauni anatokea Zanzibar, hilo nalo tusilipuuze kwa jitihada zake anazotakiwa kuzifanya.

Nchimbi yeye, anaangalia zaidi usalama wa CCM, hasa huku Tanganyika kuliko kazi maalum ya kumrudisha 'Chura' madarakani. Kwa hiyo hapa, hata kama siyo mgawanyiko ndani ya chama, lakini uzito unaelekezwa sehemu mbili tofauti kati ya hawa wawili. Na siyo hivyo tu, Nchimbi anaiona hatari kubwa zaidi kwa chama, siyo kwa serikali tu.
 
Swali nje ya swali:

Asingefariki Magu, chura kiziwi angepitishwa na chama kuwa mgombea Kisha akawa Rais 2025?

Anyway, Nchimbi naye ataonekana msaliti soon, ajiandae.
 
Sijui itakuwa bahati mbaya kiasi gani, kwamba CHADEMA safari hii fursa hii nayo iwaponyoke?

Masauni kwa kukosa busara, anawaunganisha CHADEMA ambao ilielekea walikuwa kwenye wakati mgumu hivi karibuni.
 
Swali nje ya swali:

Asingefariki Magu, chura kiziwi angepitishwa na chama kuwa mgombea Kisha akawa Rais 2025?

Anyway, Nchimbi naye ataonekana msaliti soon, ajiandae.
Hilo swali kwa upande wangu ni rahisi kulijibu. Magufuli asingeishia miaka kumi katika utawala wake.

Kuhusu Nchimbi "kuonekana msaliti". Hapana. Hali ilivyo sasa hivi ndani ya CCM chini ya Samia, hakuna anayeweza kumgusa Nchimbi, MTanganyika. Hiyo ni lulu kwa wakati huu.
 
Sijui itakuwa bahati mbaya kiasi gani, kwamba CHADEMA safari hii fursa hii nayo iwaponyoke?

Masauni kwa kukosa busara, anawaunganisha CHADEMA ambao ilielekea walikuwa kwenye wakati mgumu hivi karibuni.

..hali ni ngumu kwa vyama vya upinzani.

..havina fedha wala rasilimali za kuwezesha kuwafikia wananchi.

..hali ya kisiasa ni kama wameanza mwanzo mwaka 1993/94.
 
Mtanganyika huyu aende mbali zaidi kutetea HAKI ya kuchagua na kuchaguliwa Kwa wananchi wa ngorongoro.
 
..havina fedha wala rasilimali za kuwezesha kuwafikia wananchi.
Ni swala la kujipanga tu na kuwa na mikakati inayo eleweka. Fedha ni sehemu mhimu, lakini siyo kila kitu.
Tulipokuwa tukihimiza toka huko nyuma, miaka minne iliyo pita CHADEMA "waige" tu muundo ilio nao CCM hadi huko mitaani; haya ya kuwafikia wananchi ndiyo tuliyo kuwa tukiyalenga.
Sasa muda ndio hivyo ume yoyoma; lakini kutokana na hali nchini ilivyo wapinzani (nina maana ya CHADEMA) wakitulia vizuri; wakaacha haya yaliyokuwa yameanza kuwavuruga, mengi yakitokea CCM; nafasi ya kuibwaga CCM ni nzuri kuliko ilivyo wahi kuwepo.
Kwanza chukulia viongozi tu wakuu walioko CCM; hilo peke yake linakupa matumaini makubwa.
 
Ni watu wale wale wa CCM.
Pia ni watu wale wale wa Unguja.
Baada ya vijana wa Chadema kukamatwa,kule Unguja alikuwepo kiongozi mmoja wa CCM kwenye jukwaa anamsema kiongozi wa Upinzani, anasema," Nashangaa yule mtu ana umri wa miaka sitini lakini bado hajaoa. Tatizo ni nini? Kama hana hela za mahari mimi nitamsaidia kumpa hela za mahari.
Isipokuwa anieleze tu,anataka kuoa mwanamke au anataka kuolewa na mwanaume?"
Maneno kama yanaposenwa na viongozi wa CCM yanalets taharuki. It doesn't matter kwamba yule yupo Unguja.
Sasa tunasikitika kwamba Nchinbi anaagiza viongozi wa Chadema waachiwe. Lakini Katibu Mkuu anaongea with very little conviction,jambo ambako litawafanya Polisi wafikirie kwamba yule Katibu Mkuu hana uhakika kuhusu jambo analozungumza
Lakini Chadema wamerudia tena na tena kwamba hakuna mantiki katika kitendo cha Polisi kuwakamata viongozi wao.
 
Shida ya hawa wapinzani wanadhani kuwa mpinzani ni kutukana viongozi huwezi kila siku kumtukana kiongozi mkuu wa nchi hata kama una maoni tofauti, unaruhusiwa kupinga sera za serikali huku ukinadi sera zako. Madhara ya kutukana kiongozi kwa maana sio lazima yake matusi yetu lakini kumdharau Raisi kwa kumuita majina hata kama ni yake lakini hayatumiki kama kiongozi ni sawa kwenda kumuita Mama yako jina lake halisi badala ya Mama, hata kweli jina lake lakini utakuwa umekosa adabu na utapata unachotaka. Upinzani sio matusi upinzani pinga sera weka sera zako bila kutukana( kukosa heshima). Kiki yao ndio hii kutiwa ndani ndio wanachotaka wapate la kuongelea.
 
Enzi za Chama kimeshika Hatamu !!
Ni vyema tungerudi huko !
 
Ni kama umekatwa kichwa eeh?
 
Lakini kwa upande wa pili, Masauni naye anataka aonekane anao umwamba wa kuwatia jamba jamba CHADEMA. Tatizo ni wapi inapoishia serikali na wapi kinapo anzia chama; maana watu ni wale wale toka CCM.
Nchimbi yuko sahihi polisi wasiingilie siasa.Washughulike zaidi na matatizo ya jinai halisi ie utekaji,mauaji
 
Sasa hivi kete iliyobaki ni Nchimbi, future Presidential material. tuilinde kama mboni.
 
Haya maigizo Si mazuri.

Lissu anasumbuliwa bila sababu na mguu wake haujakaa sawa kiafya.
 
Nchimbi yuko sahihi polisi wasiingilie siasa.Washughulike zaidi na matatizo ya jinai halisi ie utekaji,mauaji
Huku CCM ikitishiwa kuondolewa madarakani?
Inaelekea wewe hujui kupangilia vipa umbele vya maswala muhimu kwa serikali na CCM yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…