Pre GE2025 Dkt. Emmanuel Nchimbi: Mkiwaona CHADEMA wanaandamana mjue wameamua kutumia miguu kufikiri

Pre GE2025 Dkt. Emmanuel Nchimbi: Mkiwaona CHADEMA wanaandamana mjue wameamua kutumia miguu kufikiri

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Vyama vya siasa vitambue kuwa dhamira ya Mazungumzo lazima iakisi pande zote, lazima iakisi ndani ya CCM na vyama vingine vya siasa, na wadau.

Kususia mazungumzo na kukwepa mazungumzo siyo ujasiri, kukimbia mazungumzo na kutaka kukwepa mazungumzo ni dalili ya uoga. Kutaka kukimbilia maandamano ni dalili ya uoga. Hoja zinajengwa kwa mdomo hazijengwi kwa miguu, hoja hazijengwi kwa maandamano.

Wakitaka kuandamana sawa sawa, hatuwezi kuwapima kwa kasi ya miguu yao, tutawapima kwa hoja zao. Vyama vya siasa lazima vijitofautishe na mashindano ya urembo, maana kwenye mashindano ya urembo tunapimana na kasi unaendaje, una staili ya kutembea.

Kweli kabisa, na hawa jamaa miguu yao ina machacha a.k.a magaga, kwa hiyo hali inazidi kuwa mbaya zaidi.

Picha hapa chini ni chadema wakiwa katika mchakato wa kufikiri.
Screenshot_20240120-174057.jpg
Screenshot_20240120-174037.jpg
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Nchimbi akizungumza na Wanachama na Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaan Leo amesema.

Mkiwaona CHADEMA wana Andamana Mjue wameamua kutumia Miguu Kufikiri Badala ya Akili/Ubongo.

View: https://www.instagram.com/reel/C2UvdMwtYtD/?igsh=ZWNpZmN3OW8wdHJq

AMEANZA VIBAYA! Bon Mayai na Martin Maranja Masese, eti tupe shule yake tuone PhD koje. Nadhani na yeye yuko kwenye lile kundi la mafisadi wa elimu alioataja Kainerugaba Msemakweli katika kitabu cha mafisadi wa elimu
Nchimbi naye yumo. leo anasema kufikiri? yeye amewahi kufikiri?
Mfano ni Makongoro Mahanga ambaye tayari ameshakwenda mahakamani kudai fidia kwa kudhalilishwa na Msemakweli. Taarifa kutoka kwenye mtandao, wengine ndani ya kitabu hicho ni Lukuvi, Mary Nagu, Kamalla,Diallo na Nchimbi.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Nchimbi akizungumza na Wanachama na Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaan Leo amesema.

Mkiwaona CHADEMA wana Andamana Mjue wameamua kutumia Miguu Kufikiri Badala ya Akili/Ubongo.

View: https://www.instagram.com/reel/C2UvdMwtYtD/?igsh=ZWNpZmN3OW8wdHJq

Matapeli ya Lumumba ndiyo yanafikiri kwa kutumia miguu. Huwezi kuuza rasilimali zote za nchi ukiwa na ubongo Sawa. Miradi yote ya kimkakati imekwama Yana akili kweli haya.? Yameuza bandari,yana akili kweli haya? Meli ya mwanza yameshindwa kukamilisha kwa wakati,Yana akili kweli haya?yameuza gesi,madini na hifadhi zetu,Yana akili kweli haya? Umeme mgawo kila siku,Yana akili kweli haya? Ni matapeli na mindevu Yao.
 
Vyama vya siasa vitambue kuwa dhamira ya Mazungumzo lazima iakisi pande zote, lazima iakisi ndani ya CCM na vyama vingine vya siasa, na wadau.

Kususia mazungumzo na kukwepa mazungumzo siyo ujasiri, kukimbia mazungumzo na kutaka kukwepa mazungumzo ni dalili ya uoga. Kutaka kukimbilia maandamano ni dalili ya uoga. Hoja zinajengwa kwa mdomo hazijengwi kwa miguu, hoja hazijengwi kwa maandamano.

Wakitaka kuandamana sawa sawa, hatuwezi kuwapima kwa kasi ya miguu yao, tutawapima kwa hoja zao. Vyama vya siasa lazima vijitofautishe na mashindano ya urembo, maana kwenye mashindano ya urembo tunapimana na kasi unaendaje, una staili ya kutembea.

View attachment 2877454
Duh..
Uwezo wa kujieleza mbona hakuna. Ila chawa wa kupiga piga makofi anao
 
Miaka 47 tangu 1977 tulipopata Katiba hii mbovu, CCM hawajawahi kupata muda wa kutosha kupata Katiba mpya, ni viraka juu ya kiraka.

Nchimbi atwambie, wanatumia nini kufikiri?
 
Miaka 60 ya uhuru hawajawahi kumaliza ujenzi wa miundombinu ukilinganisha na mkoloni aliyejenga reli Hadi Leo inatumika.

Wanatumia nini kufikiri?
 
Back
Top Bottom