Pre GE2025 Dkt. Emmanuel Nchimbi: Mkiwaona CHADEMA wanaandamana mjue wameamua kutumia miguu kufikiri

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Vyama vya siasa vitambue kuwa dhamira ya Mazungumzo lazima iakisi pande zote, lazima iakisi ndani ya CCM na vyama vingine vya siasa, na wadau.

Kususia mazungumzo na kukwepa mazungumzo siyo ujasiri, kukimbia mazungumzo na kutaka kukwepa mazungumzo ni dalili ya uoga. Kutaka kukimbilia maandamano ni dalili ya uoga. Hoja zinajengwa kwa mdomo hazijengwi kwa miguu, hoja hazijengwi kwa maandamano.

Wakitaka kuandamana sawa sawa, hatuwezi kuwapima kwa kasi ya miguu yao, tutawapima kwa hoja zao. Vyama vya siasa lazima vijitofautishe na mashindano ya urembo, maana kwenye mashindano ya urembo tunapimana na kasi unaendaje, una staili ya kutembea.

Your browser is not able to display this video.
 
Vyama vya siasa vitambue kuwa dhamira ya Mazungumzo lazima iakisi pande zote, lazima iakisi ndani ya CCM na vyama vingine vya siasa, na wadau...
Kweli kabisa
 
AMEANZA VIBAYA! Bon Mayai na Martin Maranja Masese, eti tupe shule yake tuone PhD koje. Nadhani na yeye yuko kwenye lile kundi la mafisadi wa elimu alioataja Kainerugaba Msemakweli katika kitabu cha mafisadi wa elimu
Nchimbi naye yumo. leo anasema kufikiri? yeye amewahi kufikiri?
Mfano ni Makongoro Mahanga ambaye tayari ameshakwenda mahakamani kudai fidia kwa kudhalilishwa na Msemakweli. Taarifa kutoka kwenye mtandao, wengine ndani ya kitabu hicho ni Lukuvi, Mary Nagu, Kamalla,Diallo na Nchimbi.
 
Matapeli ya Lumumba ndiyo yanafikiri kwa kutumia miguu. Huwezi kuuza rasilimali zote za nchi ukiwa na ubongo Sawa. Miradi yote ya kimkakati imekwama Yana akili kweli haya.? Yameuza bandari,yana akili kweli haya? Meli ya mwanza yameshindwa kukamilisha kwa wakati,Yana akili kweli haya?yameuza gesi,madini na hifadhi zetu,Yana akili kweli haya? Umeme mgawo kila siku,Yana akili kweli haya? Ni matapeli na mindevu Yao.
 
Duh..
Uwezo wa kujieleza mbona hakuna. Ila chawa wa kupiga piga makofi anao
 
Miaka 47 tangu 1977 tulipopata Katiba hii mbovu, CCM hawajawahi kupata muda wa kutosha kupata Katiba mpya, ni viraka juu ya kiraka.

Nchimbi atwambie, wanatumia nini kufikiri?
 
Miaka 60 ya uhuru hawajawahi kumaliza ujenzi wa miundombinu ukilinganisha na mkoloni aliyejenga reli Hadi Leo inatumika.

Wanatumia nini kufikiri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…