Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amesema wizara yake inatarajia kuunda Sheria ya Kulinda faragha za wanaotumia mawasiliano.
βData Protection Actβ itakuwa sheria kubwa ambayo ikitokea mtu anahitaji taarifa za mtumiaji basi kunakuwa na utaratibu maalumu wa kuzipata
Sheria itaeleza taarifa ambazo zinaweza kutolewa na taarifa ambazo hazipaswi kutolewa. Waziri Ndugulile amesema watafanya hayo ili kuhakikisha wanalinda faragha ya mtumiaji wa TEHAMA.
Dkt. Ndugulile amesema hii mitandao na βAppsβ ambazo watu wanatumia bure hukusanya taarifa na huwa zinauzwa kwenye makampuni ya biashara.