TANZIA Dkt. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni afariki Dunia

TANZIA Dkt. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni afariki Dunia

Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile 1969-2024

Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi", amesema.

Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, APUMZIKE KWA AMANI.

Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma,
Ofisi ya Bunge,
DODOMA.
27 Novemba, 2024


View attachment 3162859

Huu ni Msiba Mkubwa sana hasa kwa Wanachama wa JamiiForums kwa kumpoteza Mwenzao Dr Faustine Ndugulile.
View attachment 3162839
Hivi karibuni, Dk Faustine Ndugulile Jumanne ya Agosti 27, 2024 alishinda nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Ukanda wa Afrika na alipaswa kuanza majukumu hayo mapya Februari 2025.
View attachment 3162854
View attachment 3162855
View attachment 3162860
Faustine Engelbert Ndugulile, alizaliwa 31 Machi 1969) ni mwanasiasa wa chama cha CCM nchini Tanzania na ni mbunge wa jimbo la Kigamboni tangu mwaka 2010.

Mnamo 1997 alipata shahada ya udaktari wa madawa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam na mwaka 2001 alipata shahada ya uzamili katika mikrobiolojia na chanjo katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Dk Ndugulile ni nani?
DK.FAUSTINE NDUGULILEA lizaliwa March 1969 Mbulu mkoani Manyara,
Akapata elimu ya msingi na ya Sekondari nchini Zimbabwe na kisha kidato cha Tano na Sita katika shule ya Tambaza jijini Dar es Salaam.

Mwaka 1997 alipata shahada ya udaktari wa madawa katika chuo kikuu Cha Dar es salaam na mwaka 2001 alipata shahada ya uzamili ya mikrobiolojia na chanjo katika chuo kikuu Cha Dar es salaam.

Mtanzania huyu ni mwanachama wa chama cha Mapunduzi( CCM ) nchini Tanzania na ni mbunge wa jimbo la kigamboni tangu mwaka 2010.

Taaluma na kazi

Dk Ndugulile ni Daktari Tiba na ana Shahada ya Uzamili ya Tiba katika Tiba Mikrobiolojia na Kinga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shahada ya Uzamili ya Afya ya Umma (MPH) kutoka Chuo Kikuu cha Western Cape, na Shahada ya Kwanza ya Sheria (LL.B) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya ya Bunge la Tanzania, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mabunge ya Kimataifa (IPU) Advisory Group Health na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Mtandao wa Kamati za Afya za Bunge la Afrika (NEAPACOH).

Dk. Ndugulile aliwahi kuwa naibu waziri wa Afya wa Tanzania kati ya 2017-2020, pia aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 2020-2021.

Pia amefanya kazi kama mkurugenzi katika Wizara ya Afya Tanzania anayeshughulikia huduma za uchunguzi na pia meneja wa programu mwanzilishi wa Huduma ya Kitaifa ya Usambazaji Damu mwaka 2006.
Kati ya 2007-2010, aliwahi kuwa Mshauri Mkazi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) nchini Afrika Kusini akitoa msaada wa kiufundi kwa nchi nyingine nyingi kama vile Angola, Msumbiji, Tanzania na Rwanda.
Pole sana Kwa ndugu na Watanzania.R.I.P bwana Ndungulile
 
Kaka Faustine jamani, yaani huu msiba mwenzenu umenivuruga. Ni family friend. Nashindwa nampigia simu dada yake kumpa pole au naenda uwiii.
Hii familia wana roho nzuri, pamoja kuwa na pesa ila wana upendo sana. Vizuri havidumu 😭
Ulale mahala pema, peponi Kaka Faustine. Dah hee!!!
 
Duh,
Aliumwa lini? Tanzania yetu ina mambo

----

Huu utaratibu tuliojiwekea wa kutangaza kifo cha mtu tu bila kujali aliugua au ni ajali ni mbaya sana

Kwenye taarifa rasmi ya Bunge inaonesha kafariki 2025??? bahati mbaya?

Sasa jamii inabaki na mtanziko na sintofahamu kubwa..

1.Aliumwa
2 Kama aliumwa aliumwa nini na alianza lini?
3.Ajali?
4.Matibabu India ilikuwaje?
5.Chronic deaseases? Taarifa haisemi...

Ndungulile ni mtu mkubwa sana kuacha kujibu hayo maswali kwenye taarifa rasmi ya Kifo chake...

Tunaweza dhani ni jambo jema na privacy lakini minongono na 'umbea ' na 'siasa' zetu, ikatugharimu baadae...

Binafsi nilipenda sana hustle zake,

Poleni sana familia ya Dr. Faustine.

Pumzika kwa amani kaka.
Ugonjwa wa mtu ni Siri kati yake na wanaomtibia.

RIP the big boss
 
Back
Top Bottom