Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani ilikuwa ni hiyo kitu? Dadavua Kidogo....Bila kuvunja ukimya, UKIMWI utalimaliza Taifa
Bila kuvunja ukimya na sasa watu wenye maambukizi kutambulika na kuweka sera madhubuti basi Taifa litaangamia lote. Jamani ipo shida kubwa sana sana. Watu wanasambaza huu ugonjwa na wengine wana pesa. Wanasambaza kwa vijana na vijana wanasambaziana. Ukijiuliza why wanasambaza wanasambaza...www.jamiiforums.com
Sasa SI Bora ufe wewe tuh ambae hata msaada huna zaidi ya kujaza choo hapo kwa shemeji Yako,mkaza dadako.Usiishe hadi Saa100 naye aitwe kwanza
Jimbo limebak wazi kwa makondaMakonda ana dawa, anyway, alitolewa kwenye uwaziri kwa sababu ya frequent trips za kwenda India kwa matibabu.
R. I. P, kigamboni imepoteza
FOR YOUR GLORY WALKS IN HAND IN HAND WITH YOUR DOOM.Duh, Aisee.
Apumzike kwa amani Dokta Ndungulile.
Ndio mlango wa mafanikio unafunguka na milango ya kuzimu inafunguka pia.
Poleni sana ndugu na jamaa wa Dokta Ndungulile.
WdweDuh,
Aliumwa lini? Tanzania yetu ina mambo
----
Huu utaratibu tuliojiwekea wa kutangaza kifo cha mtu tu bila kujali aliugua au ni ajali ni mbaya sana
Kwenye taarifa rasmi ya Bunge inaonesha kafariki 2025??? bahati mbaya?
Sasa jamii inabaki na mtanziko na sintofahamu kubwa..
1.Aliumwa
2 Kama aliumwa aliumwa nini na alianza lini?
3.Ajali?
4.Matibabu India ilikuwaje?
5.Chronic deaseases? Taarifa haisemi...
Ndungulile ni mtu mkubwa sana kuacha kujibu hayo maswali kwenye taarifa rasmi ya Kifo chake...
Tunaweza dhani ni jambo jema na privacy lakini minongono na 'umbea ' na 'siasa' zetu, ikatugharimu baadae...
Binafsi nilipenda sana hustle zake,
Poleni sana familia ya Dr. Faustine.
Pumzika kwa amani kaka.
Utajua msibani kaa siti za nyuma nyumaChanzo cha kifo?
AiseeeeMhe. Dkt. Faustine Ndugulile 1969-2024
Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi", amesema.
Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, APUMZIKE KWA AMANI.
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma,
Ofisi ya Bunge,
DODOMA.
27 Novemba, 2024
View attachment 3162859
Huu ni Msiba Mkubwa sana hasa kwa Wanachama wa JamiiForums kwa kumpoteza Mwenzao Dr Faustine Ndugulile.
View attachment 3162839
Hivi karibuni, Dk Faustine Ndugulile Jumanne ya Agosti 27, 2024 alishinda nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Ukanda wa Afrika na alipaswa kuanza majukumu hayo mapya Februari 2025.
View attachment 3162854
View attachment 3162855
View attachment 3162860
Faustine Engelbert Ndugulile, alizaliwa 31 Machi 1969) ni mwanasiasa wa chama cha CCM nchini Tanzania na ni mbunge wa jimbo la Kigamboni tangu mwaka 2010.
Mnamo 1997 alipata shahada ya udaktari wa madawa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam na mwaka 2001 alipata shahada ya uzamili katika mikrobiolojia na chanjo katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Dk Ndugulile ni nani?
DK.FAUSTINE NDUGULILEA lizaliwa March 1969 Mbulu mkoani Manyara,
Akapata elimu ya msingi na ya Sekondari nchini Zimbabwe na kisha kidato cha Tano na Sita katika shule ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
Mwaka 1997 alipata shahada ya udaktari wa madawa katika chuo kikuu Cha Dar es salaam na mwaka 2001 alipata shahada ya uzamili ya mikrobiolojia na chanjo katika chuo kikuu Cha Dar es salaam.
Mtanzania huyu ni mwanachama wa chama cha Mapunduzi( CCM ) nchini Tanzania na ni mbunge wa jimbo la kigamboni tangu mwaka 2010.
Taaluma na kazi
Dk Ndugulile ni Daktari Tiba na ana Shahada ya Uzamili ya Tiba katika Tiba Mikrobiolojia na Kinga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shahada ya Uzamili ya Afya ya Umma (MPH) kutoka Chuo Kikuu cha Western Cape, na Shahada ya Kwanza ya Sheria (LL.B) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya ya Bunge la Tanzania, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mabunge ya Kimataifa (IPU) Advisory Group Health na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Mtandao wa Kamati za Afya za Bunge la Afrika (NEAPACOH).
Dk. Ndugulile aliwahi kuwa naibu waziri wa Afya wa Tanzania kati ya 2017-2020, pia aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 2020-2021.
Pia amefanya kazi kama mkurugenzi katika Wizara ya Afya Tanzania anayeshughulikia huduma za uchunguzi na pia meneja wa programu mwanzilishi wa Huduma ya Kitaifa ya Usambazaji Damu mwaka 2006.
Kati ya 2007-2010, aliwahi kuwa Mshauri Mkazi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) nchini Afrika Kusini akitoa msaada wa kiufundi kwa nchi nyingine nyingi kama vile Angola, Msumbiji, Tanzania na Rwanda.
Hili ni neno kubwq,sana umeojgeaHapa Tanzania ukiwa smart sana kiakili, hama nchi ukazitumie kwingine au fanya biashara kimya kimya. Don't expose your talents.
Ungesema god, ningekuelewa. Soma Romans 6:23 - karama ya Mungu ni uzima wa milele.If you hate death then logically you hate God.
Huyo jamaa sio maarufu sana kwa watanzania wengi hasa wa hali ya chini, hvy kusema hayo sio sahihi ukitaka kujua hilo em zunguka mtaani kwenye hilo jambo unalolisema utajuaHuyu mheshimiwa yawezekana alifariki siku kadhaa huko nyuma, ila kwa mambo ya siasa wameamua kutuchanganya juu kwa juu na jambo la leo.
Kwamba wakifanya yao akili za watanzania ziwe kwa marehemu.
Ukweli analitaka sana jimbo Sista PKwa Cheo alichokuwa Nacho (R.I.P) Dkt. Faustine Ndungulile asingeweza kuwa Mbunge tena acheni maneno ya kijinga na uchonganishi kama kitu haukijui subiri ueleweshwe.
Una akili Sana! Trump mwenyewe kwenye Baraza lake la mawaziri watarajiwa kampa uwaziri WA afya jamaa aliyesimama kidete kupinga chanjo za kovidiSiyo kwamba alikuwa akitumika na mabeberu - akawa anawapigia upatu? Maana ishu ya kovidi nayo ni songombingo ingine.
Hakuwa anagombea TenaDahhh. Tulisikia tetesi nyingi kuwa Bashite analitaka Jimbo lako 2025🤔
Kwahiyo walimpiga na kitu kizito mbogambogaWe're a cursed state