TANZIA Dkt. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni afariki Dunia

Poleni sana.

Dr. Ndugulile nilimjua one on one kwenye mikutano ya kuchagiza The Fourth Industrial Revolution Tanzania wakati alivyokuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia kati ya mwaka 2020 na 2021.

Nilipata kujua kuwa ana utofauti fulani na viongozi wengi, kwa kuwa alikuwa anajitahidi sana kupata maoni ya watu, kujifunza mambo mapya, kuwaweka karibu wadau wa sekta ya teknolojia na hata kuwafanya wadau ni sehemu rasmi ya kushauri policy makers.

Alianzisha mipango mizuri sana ya kuchukua maoni ya wadau kwenye mambo mapya kama Blockchain Technology na Crypto Currency.

Kwa bahati mbaya alivyoondolewa kwenye hiyo wizara, na zile outreachs zote zikaisha. Hapo ndipo wadau tukaona pengo la Dr. Ndugulile.

RIP.
 
Tunazidi kujifunza hakuna binadamu special.

Sote tutaondoka DUNIA...Nina kifua na mafua week mbili Sasa mpaka naanza kuogopa nabanja inabidi nitake serious measure.

All in all,
Kama Taifa Tumempoteza mtu SMART Sana very humble, mtu wa watu mtu makini Sanaa Dr. Faustine.

Rest easy brother.
 
Poleni sana.

Dr. Ndugulile nilimjua one on one kwenye mikutano ya kuchagiza The Fourth Industrial Revolution Tanzania wakati alivyokuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia kati ya mwaka 2020 na 2021.

Nilipata kujua kuwa ana utofauti fulani na viongozi wengi, kwa kuwa alikuwa anajitahidi sana kupata maoni ya watu, kujifunza mambo mapya, kuwaweka karibu wadau wa sekta ya teknolojia na hata kuwafanya wadau ni sehemu rasmi ya kushauri policy makers.

Alianzisha mipango mizuri sana ya kuchujua maoni ya wadau kwenye mambo mapya kama Blockchain Technology na Crypto Currency.

Kwa bahati mbaya alivyoondolewa kwenye hiyo wizara, na zile outreachs zote zikaisha. Hapo ndipo wadau tukaona pengo la Dr. Ndugulile.

RIP.
Kuna muda nakumbuka aliorganize ile zoom meeting kujadili mambo ye tech nadhan na kuhusu blockchain pia. Angeachwa kwenye hio wizara kwa muda mrefu kdg tungepata revolution kubwa sana, ndio hivyo tu hizi wizara zetu sio taasisi, hamna mipango ya muda mrefu bali kila anaeingia anakuana plan yake badala ya kuwa msimamizi wa mipango ya muda mrefu
 
Tanzia

View attachment 3162827

Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi", amesema.

Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, APUMZIKE KWA AMANI.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma,
Ofisi ya Bunge,
DODOMA.
27 Novemba, 2024
sumu huua taratibu.DAB
 
Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile 1969-2024

Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi", amesema.

Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, APUMZIKE KWA AMANI.

Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma,
Ofisi ya Bunge,
DODOMA.
27 Novemba, 2024

View attachment 3162859

Huu ni Msiba Mkubwa sana hasa kwa Wanachama wa JamiiForums kwa kumpoteza Mwenzao Dr Faustine Ndugulile.
View attachment 3162839
Hivi karibuni, Dk Faustine Ndugulile Jumanne ya Agosti 27, 2024 alishinda nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Ukanda wa Afrika na alipaswa kuanza majukumu hayo mapya Februari 2025.
View attachment 3162854
View attachment 3162855
View attachment 3162860
Faustine Engelbert Ndugulile, alizaliwa 31 Machi 1969) ni mwanasiasa wa chama cha CCM nchini Tanzania na ni mbunge wa jimbo la Kigamboni tangu mwaka 2010.

Mnamo 1997 alipata shahada ya udaktari wa madawa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam na mwaka 2001 alipata shahada ya uzamili katika mikrobiolojia na chanjo katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Dk Ndugulile ni nani?
DK.FAUSTINE NDUGULILEA lizaliwa March 1969 Mbulu mkoani Manyara,
Akapata elimu ya msingi na ya Sekondari nchini Zimbabwe na kisha kidato cha Tano na Sita katika shule ya Tambaza jijini Dar es Salaam.

Mwaka 1997 alipata shahada ya udaktari wa madawa katika chuo kikuu Cha Dar es salaam na mwaka 2001 alipata shahada ya uzamili ya mikrobiolojia na chanjo katika chuo kikuu Cha Dar es salaam.

Mtanzania huyu ni mwanachama wa chama cha Mapunduzi( CCM ) nchini Tanzania na ni mbunge wa jimbo la kigamboni tangu mwaka 2010.

Taaluma na kazi

Dk Ndugulile ni Daktari Tiba na ana Shahada ya Uzamili ya Tiba katika Tiba Mikrobiolojia na Kinga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shahada ya Uzamili ya Afya ya Umma (MPH) kutoka Chuo Kikuu cha Western Cape, na Shahada ya Kwanza ya Sheria (LL.B) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya ya Bunge la Tanzania, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mabunge ya Kimataifa (IPU) Advisory Group Health na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Mtandao wa Kamati za Afya za Bunge la Afrika (NEAPACOH).

Dk. Ndugulile aliwahi kuwa naibu waziri wa Afya wa Tanzania kati ya 2017-2020, pia aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 2020-2021.

Pia amefanya kazi kama mkurugenzi katika Wizara ya Afya Tanzania anayeshughulikia huduma za uchunguzi na pia meneja wa programu mwanzilishi wa Huduma ya Kitaifa ya Usambazaji Damu mwaka 2006.
Kati ya 2007-2010, aliwahi kuwa Mshauri Mkazi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) nchini Afrika Kusini akitoa msaada wa kiufundi kwa nchi nyingine nyingi kama vile Angola, Msumbiji, Tanzania na Rwanda.

Poleni sana wafiwa wote. RIEP Dr. Faustine. Long ago we met ulipokuwa unasoma. Sikujua kama ungechagua political path one day.

Sad that you have gone at the pinnacle of your career. It is something that we all have nothing about to make a decision. When death comes, hakuna namna tunaweza kukwepa. Hata siku ya kupiga kura, kifo kinaweza kuja tu.

Death, as it is, is one of the ultimate and powerful tool which make all the creatures of the world, equal and the same.
 
Watu makini wameondoka na mwezi November. Lokole, Mengele na others alike wana dunda tu
 
Makonda ana dawa, anyway, alitolewa kwenye uwaziri kwa sababu ya frequent trips za kwenda India kwa matibabu.

R. I. P, kigamboni imepoteza
Kigamboni imepoteza nini!? Hatujapoteza chochote, marehemu ni mtu tu kama wengine, huku kigamboni kila siku wanakufa watu, tunazika kila siku ziendazo kwa mungu.
Nafasi yake atapatikana mwingine..
Yale mema aliyofanya atakumbukwa kwa mema hayo na alipokosea waliobaki duniani wamsamehe, binadamu sote mwisho wetu ni mmoja
Tuishi kwa wema tutende mema, tusiishi kama hapa duniani tutabaki daima

Kila nafsi ITAONJA umauti.
 
Poleni sana wafiwa wote. RIEP Dr. Faustine. Long ago we met ulipokuwa unasoma. Sikujua kama ungechagua political path one day.

Sad that you have gone at the pinnacle of your career. It is something that we all have nothing about to make a decision. When death comes, hakuna namna tunaweza kukwepa. Hata siku ya kupiga kura, kifo kinaweza kuja tu.

Death, as it is, is one of the ultimate and powerful tool which make all the creatures of the world, equal and the same.
Sad truth!!
 
Back
Top Bottom