TANZIA Dkt. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni afariki Dunia

TANZIA Dkt. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni afariki Dunia

Hivi Huwa Kuna nini!?nyuso za Hawa wakuu Huwa kama Zimefanyiwa plastic surgery vile!!?

Yaani USO kama umewekewa puto fulani hivi!!?

Mbona juzi mafuru Leo huyu jamaa!!

Mbona wanaenda huko kwa kasi!!?
 
Kama jimbo ameshasema ataliachia mwezi February 2025 atakapokwenda kuanza rasmi majukumu yake mapya huko WHO lakini nafikiri kuna jitu limeona huko ni mbali sana!
Naomba unikumbushe ali-compete na nani 2020 na tofauti yao ya kura ilikuwaje??

Je huyo ali-compete naye yuko katika position ya kugombea????
 
Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile 1969-2024

Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi", amesema.

Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, APUMZIKE KWA AMANI.

Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma,
Ofisi ya Bunge,
DODOMA.
27 Novemba, 2024


View attachment 3162859

Huu ni Msiba Mkubwa sana hasa kwa Wanachama wa JamiiForums kwa kumpoteza Mwenzao Dr Faustine Ndugulile.
View attachment 3162839
Hivi karibuni, Dk Faustine Ndugulile Jumanne ya Agosti 27, 2024 alishinda nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Ukanda wa Afrika na alipaswa kuanza majukumu hayo mapya Februari 2025.
View attachment 3162854
View attachment 3162855
View attachment 3162860
Faustine Engelbert Ndugulile, alizaliwa 31 Machi 1969) ni mwanasiasa wa chama cha CCM nchini Tanzania na ni mbunge wa jimbo la Kigamboni tangu mwaka 2010.

Mnamo 1997 alipata shahada ya udaktari wa madawa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam na mwaka 2001 alipata shahada ya uzamili katika mikrobiolojia na chanjo katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Dk Ndugulile ni nani?
DK.FAUSTINE NDUGULILEA lizaliwa March 1969 Mbulu mkoani Manyara,Akapata elimu ya msingi na ya Sekondari nchini Zimbabwe na kisha kidato cha Tano na Sita katika shule ya Tambaza jijini Dar es Salaam.

Mwaka 1997 alipata shahada ya udaktari wa madawa katika chuo kikuu Cha Dar es salaam na mwaka 2001 alipata shahada ya uzamili ya mikrobiolojia na chanjo katika chuo kikuu Cha Dar es salaam.

Mtanzania huyu ni mwanachama wa chama cha Mapunduzi( CCM ) nchini Tanzania na ni mbunge wa jimbo la kigamboni tangu mwaka 2010.

Taaluma na kazi

Dk Ndugulile ni Daktari Tiba na ana Shahada ya Uzamili ya Tiba katika Tiba Mikrobiolojia na Kinga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shahada ya Uzamili ya Afya ya Umma (MPH) kutoka Chuo Kikuu cha Western Cape, na Shahada ya Kwanza ya Sheria (LL.B) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya ya Bunge la Tanzania, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mabunge ya Kimataifa (IPU) Advisory Group Health na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Mtandao wa Kamati za Afya za Bunge la Afrika (NEAPACOH).

Dk. Ndugulile aliwahi kuwa naibu waziri wa Afya wa Tanzania kati ya 2017-2020, pia aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 2020-2021.

Pia amefanya kazi kama mkurugenzi katika Wizara ya Afya Tanzania anayeshughulikia huduma za uchunguzi na pia meneja wa programu mwanzilishi wa Huduma ya Kitaifa ya Usambazaji Damu mwaka 2006.
Kati ya 2007-2010, aliwahi kuwa Mshauri Mkazi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) nchini Afrika Kusini akitoa msaada wa kiufundi kwa nchi nyingine nyingi kama vile Angola, Msumbiji, Tanzania na Rwanda.

APUMZIKE KWA AMANI
NINI SABABU YA KIFO CHA KAKA YETU DKT FAUSTINE?
 
Hapo JKCI/MNH ina maana wanacheza cheza tu, maana wakubwa wote wanaenda India na kurudi kama cargo.
Hapana Jkci wakishindwa ujue hiyo tayari imeshakuwa ni safari ya one way ticket !
Huko India ni kwenda kujaribu bahati tu ! 🙏

After all kufa ni lazima sote tutakufa hata wale mahodari wa kudhalilisha wengine nao watakufa tu !
Hata wale wenye kutanguliza wengine nao watakufa tu tena ni baada ya kuteseka sana mu Dunia ndipo watakapotwaliwa 🙏 !
 
Back
Top Bottom