Dkt. Fred Msemwa: Watanzania Milioni 1.174 walitoa maoni ya ana kwa ana kupitia Kaya zao

Dkt. Fred Msemwa: Watanzania Milioni 1.174 walitoa maoni ya ana kwa ana kupitia Kaya zao

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango Dkt. Fred Msemwa ameeleza ufanisi uliotumika wa ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Dira ya Taifa 2050, akieleza kuwa walitumia njia shirikishi kufikia wananchi moja kwa moja. Amesema zaidi ya Watanzania milioni 1 walitoa maoni yao ana kwa ana kupitia utaratibu wa kaya kwa kaya

"Kazi ya kukusanya maoni imefanyika kwa ufanisi mkubwa, tulitumia njia mbalimbali katika kuhakikisha kila Mtanzania popote alipo anaweza kutoa maoni. Tulipita Kaya kwa Kaya, Nyumba kwa Nyumba ambapo tulikuwa na madodoso ili kuuliza Wananchi wenzetu juu ya maoni yao kuhusu Dira na matamanio yao ya namna wanavyotaka nchi yetu iwe itakapofika mwaka 2050"

"Kupitia utaratibu huo Mhe. Rais tuliweza kuwafikia Watanzania Milioni 1.174 ambao walitoa maoni ya ana kwa ana kupitia Kaya zao"


 
A waste of resources (time and money). Kutengeneza dira sio mchakato wa kisiasa, hivyo hauhitaji kupata consensus ya watu wengi....unahitaji inputs za watu wachache wenye utaalamu kwenye nyanja zao kitaaluma/kazi na maono ya mbeleni.....
 
Back
Top Bottom