PreGE2025 Dkt. Godwin Mollel Awapatanisha Viongozi wa Kimasai kwa Ajili ya Umoja na Mshikamano

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708

Your browser is not able to display this video.
Mbunge wa Jimbo la Siha na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amewapatanisha viongozi wa Kijamii wa Kimasai, Ole Paserian na Ole Kisongo, na kuimarisha mshikamano ndani ya jamii hiyo.

Hafla hiyo imefanyika wakati wa ibada ya kubariki "Malaiyoni" (watoto wa Kimasai) kabla ya kufanyiwa tohara, ikiwa ni sehemu ya desturi na tamaduni za jamii ya Kimasai, ambapo katika tukio hilo, Viongozi wa pande zote wamekubaliana kushirikiana kwa ajili ya ustawi wa jamii yao.

Dkt. Mollel amesisitiza umuhimu wa mshikamano na amani katika jamii, akisema kuwa umoja ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiafya.

Aidha, amesema “Tunaakikisha watoto hawapotezi Mila yao pia wanapenda Mila yao , tunawatayarisha kuwa Morani , hii ni hatua ya kwanza kuelekea kufikia hatua ya Tatu Itakayowafanya kuwa Morani.”
Your browser is not able to display this video.


​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…