Mbunge wa Jimbo la Siha (CCM), Dkt. Godwin Mollel, ametabiri anguko na kifo cha kisiasa cha chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA, akidai kuwa safu yake mpya ya uongozi wakuu haina uwezo wa kiutawala bali inaendeshwa na itikadi za kianaharakati na makelele ya jukwaani.
Akizungumza katika mahojiano maalum na televisheni ya mtandao ya Manyunyu TV leo Jumanne, Juni 9, 2026, Dkt. Mollel ameweka wazi kuwa viongozi hao hawana sifa za kuingia Ikulu kwasababu hawakupitia mfumo rasmi wa kujengwa kiuongozi, jambo litakalosababisha chama hicho kuendelea kushuka na kupoteza ushawishi kwa wananchi.
Alijinasibu kuwa CCM ina mifumo imara kuanzia chipukizi mpaka Umoja wa Vijana (UVCCM), tofauti na upinzani ambapo mtu anaweza akawa hajulikani lakini akionekana tu "amependeza" jukwaani na ana uwezo wa kuongea anapewa uongozi bila kujali kesho atafanya nini