PreGE2025 Dkt.Godwin Mollel: Wapinzani wangu Jimboni nimewanyoosha hadi sasa wamebaki kutumia vibaraka wao

PreGE2025 Dkt.Godwin Mollel: Wapinzani wangu Jimboni nimewanyoosha hadi sasa wamebaki kutumia vibaraka wao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Snapinst.app_485259282_1518880095752866_6415721766107072368_n_1080.jpg

Alichoandika Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Siha, Dkt.Godwin Mollel kwenye ukurasa wake wa Instagram:

Hapa nilikuwa namwambia boss, wapinzani wangu jimboni nimewanyoosha hadi sasa wamebaki kutumia vibaraka wao waliopo kamati ya siasa kumlazimisha Katibu CCM wa Wilaya kuandika barua za vitisho na hata hoja kwenye barua yenyewe hamna.

Mara ooh... unasumbua wazee wa chama, wazee wenyewe nimewapokonya milioni 316 walizotaka kupora ushirika wa Siha Kiyeyu, pia sasa wanalipa zaidi ya milioni 200 ambazo hazionekani.

Na wengine nimewafurumusha nikiwa na Wananchi 700 na madiwani wakiiba ardhi ya Siha kuwekeza kitapeli, ambao walitaka kuuza ardhi ya leoni, sisi na madiwani tuliowafukuza mafisadi hawa tumeandikiwa barua ya kamati ya nidham

Kicheko...! Hivi kwa akili ya kawaida anaeitwa polisi ni mwizi au mfukuza mwizi, ilibidi tucheke sanaaaaa...

Kwasababu kinachosikitisha sisi tuliofukuza wezi ndo tunaitwa kwenye kamati ya nidhamu ilhali wazee waliouza ndo wametushitaki kuwa ndo tuna makosa, na kamati hiyo ya siasa inajua fika kua hao wazee ndo wabadhirifu, na wizara ya kilimo inajua p na vyombo vimethibitisha na document zipo

Boss ameniambia Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka rasilimali za wasiha zilindwe kwa gharama yoyote, na ameniambia anakuja siha mwezi wa 5 kuongeza nguvu kwenye ulinzi wa rasilimali za wasiha.

Nimemuomba ruhusa niingie Siha kuanzia ijumaa ili niwanyooshe hadi jumanne nirud bungeni.

Screenshot 2025-03-20 200725.png
 
Wachache wanakuw matajiri wengi wanakufa masikini uku matajiri wakijisifu kuwasaidia masikini wanaokufa
 
Back
Top Bottom