Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe amesema watu 281 wakiwemo watumishi wa afya 64 waliokuwa wametangamana na wagonjwa wa Marburg mkoani Kagera, wametoka karantini wakiwa salama.
Amesema katika mipaka ikiwemo viwanja vya ndege na bandari, wasafiri 18 kati ya 417,148 waliochunguzwa, walihisiwa kuwa na ugonjwa wa Marburg, lakini baada ya uchunguzi wa kina walibainika kuwa na magonjwa mengine ambayo tayari yametibiwa.