Dkt. Gwajima: Vitendo vya Ubakaji na Ulawiti vimepungua kwa asilimia 6.3 na 19 mwaka 2024

Dkt. Gwajima: Vitendo vya Ubakaji na Ulawiti vimepungua kwa asilimia 6.3 na 19 mwaka 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini vimeanza kupungua, hususan matukio ya ubakaji na ulawiti, kufuatia juhudi mbalimbali za Serikali na wadau kuelimisha jamii.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025/26 jijini Dodoma leo, Dkt. Gwajima alieleza kuwa matukio ya ubakaji yamepungua kutoka 8,185 mwaka 2023 hadi kufikia 7,670 mwaka 2024, ikiwa ni punguzo la asilimia 6.3.

Aidha, aliongeza kuwa matukio ya ulawiti nayo yamepungua kutoka 2,382 mwaka 2023 hadi 1,930 mwaka 2024, sawa na upungufu wa asilimia 19, hatua inayodhihirisha maendeleo ya harakati za kupambana na vitendo hivyo nchini.

 
Back
Top Bottom