Dkt. Homera akutana na watendaji wa kampuni ya Vivo Energy

Dkt. Homera akutana na watendaji wa kampuni ya Vivo Energy

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
๐——๐—ž๐—ง. ๐—›๐—ข๐— ๐—˜๐—ฅ๐—” ๐—”๐—ž๐—จ๐—ง๐—”๐—ก๐—” ๐—ก๐—” ๐—ช๐—”๐—ง๐—˜๐—ก๐——๐—”๐—๐—œ ๐—ช๐—” ๐—ž๐—”๐— ๐—ฃ๐—จ๐—ก๐—œ ๐—ฌ๐—” ๐—ฉ๐—œ๐—ฉ๐—ข ๐—˜๐—ก๐—˜๐—ฅ๐—š๐—ฌ

โ–ช๏ธ๐—ฌ๐—ฎ๐—ผ๐—ป๐—ฒ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ป๐—ถ๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜„๐—ฒ๐—ธ๐—ฒ๐˜‡๐—ฎ ๐—ธ๐—ฎ๐˜๐—ถ๐—ธ๐—ฎ ๐—ก๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ๐˜๐—ถ ๐—ฆ๐—ฎ๐—ณ๐—ถ ๐˜†๐—ฎ ๐—ž๐˜‚๐—ฝ๐—ถ๐—ธ๐—ถ๐—ฎ ๐——๐—ฎ๐—ฟ ๐—ฒ๐˜€ ๐—ฆ๐—ฎ๐—น๐—ฎ๐—ฎ๐—บ.

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, Oktoba 22, 2026, amekutana na watendaji wa Kampuni ya Vivo Energy inayojishughulisha na usambazaji wa mafuta na vilainishi katika nchi mbalimbali duniani, ambapo wamejadili masuala ya uwekezaji, ikiwemo nia ya kampuni hiyo kupanua shughuli zake nchini Tanzania.

Katika mazungumzo hayo, Mtendaji wa Kampuni ya Vivo Energy nchini Tanzania, Mohamed Bougriba, amemweleza Dkt. Homera kuwa kampuni hiyo ina nia ya kupanua wigo wa uwekezaji wake kwa kujikita katika sekta nyingine, zikiwemo maji, madini na nishati safi ya kupikia.

Dkt. Homera ameipongeza kampuni hiyo kwa shughuli zake za usambazaji wa mafuta na vilainishi pamoja na kuonesha nia ya kuwekeza katika nishati safi ya kupikia, akieleza kuwa uwekezaji huo utachangia juhudi za Serikali za kufikia lengo la asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.
 

Attachments

  • publer-1792726593303.jpg
    publer-1792726593303.jpg
    56.7 KB · Views: 2
  • publer-1792726597640.jpg
    publer-1792726597640.jpg
    66.3 KB · Views: 4
  • publer-1792726596531.jpg
    publer-1792726596531.jpg
    65.5 KB · Views: 3
  • publer-1792726595304.jpg
    publer-1792726595304.jpg
    60.7 KB · Views: 2
Back
Top Bottom