Zanzibar 2020 Dkt. Hussen Mwinyi: Tumaini linalorejea Zanzibar

Zanzibar 2020 Dkt. Hussen Mwinyi: Tumaini linalorejea Zanzibar

Mtoto wa mwinyi anataka urais Zanzibar,mtoto wa karume anataka urais Zanzibar na mtoto wa abood Jumbe naye anataka urais Zanzibar. Hii kitu inaitwa Nini?
hiyo yaitwa kuwafanya wenzenu mazezeta, mazwazwa na mazumbukuku yaani hizo familia wanajiona wao tu ndio bora kuliko mtu yoyote Zenji na wana hati miliki ya kutawala nchi!!

ala ala mti na macho wazenji tusifanye makosa twende na Jecha hana makundi, hana kambi , hana makuu, ni mkazi na mwenyeji mwenzetu, ni mzoefu wa uongozi nafasi za juu, ni mtu ana uwezo binafsi wa kutoa maamuzi magumu bila kujali umma utachukuliaje kama pale aliwatoroka kamati na kujificha chini ya uvungu akamtangaza Rais peke yake kibabe!

Jecha ni jeshi la mtu mmoja ndie Magu wa Zenji ni jasiri ni mbabe ana hekima na busara na umri sahihi kuongoza visiwani!! huyu pekee ataulinda muungano sababu keshafanya kwa vitendo yale ya kuulinda! kwakuwa wazenji wamemzingua kumjazia form zake za udhamin wa urais ana usongo nao mno na ndie anafaa urais awakomeshe wote wenye fyokofyoko na waliotulia Zenji kwa maslahi mapana ya bara!!kukiwa na vita kati ya Jecha na raia ni faida ya kunguru!!

kamati kuu Lumumba msikosee kujali dhahabu hii inaitwa Mr Jecha hana kambi , hana makuu!! wagombea wengine wote ni wachumia tumbo tu!! sie wengine tuko pembezoni ila tunaona mbali mno!!! watu hubadilika wakipewa madaraka makubwa mfano Magu hakuna mtu alimfahamu kuwa atakuwa Rais wa hivi akiwa waziri , na hata ccm iwe makini na chagu lake huko Zenj!!! kina Slow times two msijesema hatukuwashtueni!!
 
Ya kazi ya kukulisha mavi dada bunyero.
kila goti litapigwa na kila yakhe mla mapembe na chaza ati, wewe subiri tumpe Jecha rungu lake awanyooshe wote nyie, hii inaitwa kizungu DIVIDE AND RULE! sijaona hoja yako zaidi ya povu tu , kwani bibie umechukia nini ati? ushalipiwa weye!!
 
kila goti litapigwa na kila yakhe mla mapembe na chaza ati, wewe subiri tumpe Jecha rungu lake awanyooshe wote nyie, hii inaitwa kizungu DIVIDE AND RULE! sijaona hoja yako zaidi ya povu tu , kwani bibie umechukia nini ati? ushalipiwa weye!!
Naona unatafuta basha kwa nguvu,kaoshe kwanza puru then urudi hapa jamvini upewe protin za moto mtoto. Mzuri.
 
Hujaskia majimbo ma 4 yemefutwa?
Wazanzibari waliuondoa Usultani,Walifanya Mapinduzi kuondoa thulma ya kuridhishana uongozi kifamilia...

Sasa CCM Zanzibar wanataka kuuendeleza Usultani kwa style Yao..

Zanzibar Safari iende upinzani,ACT,CDM au chama chengine Cha siasa lakini sio CCM
 
Samahani kabla sijachangia Deogratius Mutungi, wewe una uhusiano na mkuu wa usajili wa vyama Jaji Mutungi?

Isije ikawa tiyari una majibu ya uchaguzi kabla ya uchaguzi, sisi tukaumiza vidole gumba kwa kubofya, keyboards..

Everyday is Saturday... 😎
hapana majina yanafanana tu wala hawana husiano wowote huyu ni mwanishi wa habari na msomi wa udsm;
 
DKT HUSSEN MWINYI TUMAINI LINALOREJEA ZANZIBAR

Na, Deogratias Mutungi

Nianze makala haya kwa kusema Zanzibar na Wazanzibar kwa ujumla wake awamu hii wanaweza kupata kiongozi aliye bora zaidi na mwenye maono ya pekee katika ukombozi wa Mzanzibar mwenyewe dhana hii inajengwa kutokana na waliojitokeza kuchukua fomu ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kuwa wagombea wenye sifa zilizotukuka kiuongozi kiitikadi, kiimani na kitaaluma.

Hata hivyo maudhui ya “Tumaini linalorejea” ni nadharia kuwa maisha ya binadamu ni mapambano, ni mwenye uthubutu tu ndiye hatimaye hushinda aidha njia ya kuelekea ushindi siyo lazima iwe imenyooka, kuna wakati inapinda na kuna wakati inakuwa na vizingiti na wakati mwingine fumbo linakuwa halijafunguliwa na kutunza lengo ni sehemu ya kudumisha tumaini na hatimaye likarejea kwenye njia iliyochaguliwa na ushindi kwenda kwa kwa mstahiki. Na sasa makala haya yanasema tumaini linalorejea Zanzibar hatimaye limepatikana.

Ikumbukwe kuwa kama taifa tupo kwenye kipindi na hatua muhimu kidemokrasia wakati tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo Oktoba mwaka huu, Kama ilivyo desturi na taratibu ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM utaratibu wa ndani unaendelea ili kumpata kiongozi mwenye uwezo, uthubutu na misimamo isiyoteteleka katika nafasi ya Urais ili kukabiliana na changamoto za kimaendeleo ndani ya nchi na katika anga za kidiplomasia.

Makala haya kwa ufanisi wa hali ya juu yanaelekeza jicho lake la uchambuzi wa kisiasa kwa kumulika siasa za Zanzibar hasa katika nyakati hizi za kuwania nafasi mbalimbali za kiuongozi, aidha makala haya yanaangaza uwezo, weledi na utendaji kazi wa wagombea waliochukua fomu kuomba ridhaa ya ndani ya chama kutoa nafasi kwao kuwapa fursa kama wagombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM.

Tumesikia na kuona waliojitokeza ni wengi na wenye uwezo, sifa na uzoefu wa kutosha katika siasa za Tanzania bara na Visiwani Zanzibar kwa kuomba ridhaa ya kupewa nafasi hiyo muhimu kisiasa, lakini mantiki inaonyesha kati ya wengi waliojitokeza ni Dkt. Husseni Mwinyi tu mwenye sifa za upekee na utofauti wa aina yake anayestahili kupewa nafasi ya kuwa Urais wa Zanzibar na si vinginevyo, Wala huu si upendeleo bali ni ukweli wa kimantiki unaotumia mifumo ya kisiasa kumtambua mtu kulingana na sifa zake za kiuongozi, Kwa dhana hiyo uwajibikaji aliouonyesha Dkt. Mwinyi kwenye nafasi ya uwaziri unambeba sana ukilinganisha na wagombea wengine.

Kimantiki na kisiasa Dkt. Mwinyi ni tumaini linalorejea Zanzibar kuikomboa Zanzibar kifalsafa, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni, Upekee wa kiuongozi kwa Dkt. Mwinyi unasimama katika falsafa ya weledi, utashi, misimamo na maamuzi ikiwa ni pamoja na kuiva kiitikadi na kitaaluma “red and expert” bila shaka hili halina ubishi wa aina yoyote na ni imani ya makala haya kuwa hakuna wa kuhoji juu ya dhana hii dhidi ya Dkt. Mwinyi. Aidha mbali na wagombea wenzake ndani ya Chama Cha Mapinduzi kutomfikia kiuwezo katika nadharia ya uongozi lakni bado Dkt. Husseni Mwinyi huwezi kumliganisha na mgombea wa chama chochote cha kisiasa hasa upinzani ndani ya Zanzibar na viunga vyake.

Pengine tujiulize ni kwanini halinganishwi na upande wa pili katika siasa za upinzani, Sababu kuu naya msingi ni moja tu ambayo ni kuwa Dkt. Mwinyi ni kiongozi mwenye msimamo wa kutetea hoja yake, Yuko tayari kusikiliza hoja mpya na kuzikubali kama hoja hizo zitakuwa zina maslahi kwa watu badala ya maslahi kwa makundi au mtu binafsi.

Mathalani kisiasa uwezi ukamlinganisha Dkt. Mwinyi na Mgombea wa ACT-Wazalendo Maalim Seif Sharrif Hammad viongozi hawa wawili ukiwaweka kwenye mizania ili kutafuta ulali wao kisiasa bado Dkt. Husseni Mwinyi anampita kwa mbali sana Maalim Seif Sharrif Hammad, nafikri hata angeulizwa Maalim mwenye angekiri mashiko ya hoja hii na ukweli wake.

Lakini zipo sababu zinazowatofautisha nazo ni busara, upeo, tamaa ya madaraka na unyeyekevu kwa watu, kama makala haya yangetoa asilimia dhidi ya viongozi hawa basi Dkt. Mwinyi angepata 96% dhidi ya Maalim ambaye angepata 50% kwa mantiki hiyo Mwinyi ni kiongozi anayeweza na mwenye sifa zilizotukuka na za upekee katika uongozi ndani ya taifa letu.

Ikumbukwe kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM kilianza kufanya kazi za kuainisha sifa za mgombea nafasi ya Urais mwaka 1985 wakati Mwl. Nyerere anang’atuka zilitungwa sifa thelathini na tano, ikaendelea hivyo hivyo kwa awamu zilizofuatia ikiwa ni pamoja na 1995, 2005, 2010, 2015

Na miongoni mwa sifa za mgombea Urais zilizotajwa na kuorodheshwa ni pamoja na; Kuwa na upeo wa kuona mbali, Asiyeyumbishwa katika msimamo wa kufanya maamuzi, Awe na uzoefu wa kuongoza, Awe mwadilifu, Asiependa kusikiliza majungu, Awe na elimu ya Chuo Kikuu, Asiwe na tamaa ya kujilimbikizia mali, Achukie rushwa, Asiwe mbinafsi na Asiwe Mbaguzi, hizi ni miongoni mwa sifa zinazomtambulisha mgombea wa CCM kuwa safi na mwenye kustahili kupata nafasi ya kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi.

Bila shaka Dkt. Husseni Mwinyi ndiye kiongozi mwenye sifa zilizoainishwa hapo juu na ndiye anayestahili kwa vyovyote vile kuipeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi, Waswahili wanasema “Mnyonge myongeni lakini haki yake mpeni, tunahitaji kumpa nafasi Dkt. Mwinyi kuivusha Zanzibar kutoka hapa ilipo, ni kiongozi mwenye falsafa za kimapinduzi na mabadiliko katika kuwatumikia Wazanzibar, aidha ni kiongozi mwenye kutumia busara kufikia maamuzi yenye tija kwa watu na maendeleo yao.

Katika maandiko matakatifu ya dini ya Massiha (Yesu Kristo) kuna msemo usemao “Wanyenyekevu watarithi na kutawala dunia” Msemo huu wa maandiko matakatifu ni msemo ambao pamoja na mambo mengine unaelezea watu wa haiba ya Dkt. Husseni Mwinyi kwa vipi wanazingatia maadili ya chama na utii kwa viongozi na wazee bila kuuza roho yake kwa shetani, Si rahisi kujua lini Dkt. Mwinyi ana jambo linalomsumbua mpaka limemsumbua kweli.

Kwa muda mwingi Dkt. Husseni Mwinyi hutuliza roho yake kwa tabasamu na kukakataa kuzama katika sononeko, Tabia yake hiyo imemsaidia kutoweka fundo rohoni na vilevile kuwafanya marafiki na maadui zake wasijue kusudio lake wakati uliopo na pale anapobaini kwamba “ huu ndio muda muafaka” husema bila kificho wala woga chochote kile kilichopo rohoni mwake.

Kwa tabia hizo na hulka za namna hiyo kisiasa unaweza kumfananisha Dkt. Husseni Mwinyi na rais wa zamani wa Afrika Kusini, mzee Nelson Mandela ufanano wao unaanzia kwenye dhana ya hulka na utendaji kazi, Mandela alikuwa mpole na mwepesi wa kuzikiliza shida za watu wake, Mandela alisimamia mrengo wa kuwaunganisha watu na kuwaleta pamoja bila ubaguzi wa aina yoyote, ndivyo ilivyo kwa Dkt. Husseni Mwinyi ni kiongozi mwenye utashi wa kusikiliza na kutatua kero za watu zinazowakabili ili kuwakomboa pale walipokwama, Mandela na Mwinyi wote kwa pamoja wanaunganishwa na falsafa chanya kwa kuwa na fikra za kumkomboa myonge anayeonewa.

Kwa lugha nyepesi ya kisiasa ni vigumu kutenganisha hulka na tabia za Mzee Mandela na Dkt. Husseni Mwinyi, kama hivyo ndivyo basi Chama Cha Mapinduzi CCM kimpe fursa mgombea huyu aweze kufata nyayo za pacha wake mzee wetu Nelson Mandela kwa kuwaletea Wazanzibar ustawi wa maendeleo uliotukuka, Ni Imani ya makala haya kuwa Mwinyi atatenda na kufata yale yote ambayo Nelson Mandela aliwatendea wana Afrika Kusini na kuacha alama iliyotukuka, tuna imani na Dkt. Mwinyi kuwa atapata nafasi ya Urais na hatimaye atatenda na kuacha alama kwa Wazanzibar.

Aidha Dkt. Husseni Mwinyi anatambua kuwa Zanzibar inakabiliwa na changamoto lukuki hasa katika maeneo ya ajira, muungano na uchumi wa mtu mmoja mmoja pia ameishi na kulelewa katika mazingira ya kizanzibar hivyo basi anaelewa fika na kutambua changamoto hizo na ni kwa namna gani anaweza kuzitatua hili kuboresha maisha ya Wazanzibar, Kwa dhana hizo Dkt. Mwinyi ni chaguo tosha kwa Chama Cha Mapinduzi CCM katika kuhakikisha anapeperusha vyema bendera ya chama katika kinyanganyiro cha uchaguzi mkuu hapo Oktoba.

dmutunid@yahoo.com
Kennedy family,mbarawa kuingia tatu bora
 
Hongera kwa andiko zuri kaka nikweli umeetueleza sifa nzuri za mhe Dr ila sijaona ulipo tuelezea udhaifu na changamoto zake
 
Back
Top Bottom