Mwaka 1960, Jane Goodall alienda Gombe (iliyokuwa game reserve ndogo kando ya Ziwa Tanganyika, Kigoma). Mwaka 1968 ikawa Hifadhi ya Taifa Gombe Stream – ili kulinda sokwe na kuruhusu utafiti wa kudumu.
Gombe imekuwa maabara ya asili (open-air laboratory) kwa zaidi ya miaka 65 sasa.
Jane Goodall alipoona uharibifu wa misitu jirani na Gombe, alihamasika kuanzisha Jane Goodall Institute (JGI).
JGI ilianzisha miradi ya uhifadhi inayojumuisha wakazi wa vijiji karibu na Gombe:
TACARE (Lake Tanganyika Catchment Reforestation and Education Project) – kusaidia jamii kulinda misitu kwa njia endelevu.
Kupanda miti na kurejesha misitu iliyoharibiwa.
Elimu ya mazingira kwa vijana kupitia programu ya Roots & Shoots.(ambayo kwa njia moja ama nyingine nilinufaika nayo na wanafunzi walio wengi pia )
Tanzania ilimtambua rasmi 2017, kama sehemu ya kusherehekea miaka 56 ya utafiti wake wa sokwe wa Gombe, ambapo serikali ikamwonyesha heshima kwa michango yake kwenye uhifadhi wa wanyamapori. (Umaarufu wote tunaouna gombe ulichangiwa na tafiti za huyu mama majarida ya national geographil nk yaliiongelea Gombe sababu ya tafiti za huyu mama
Mwaka 2006, Chuo Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania) kilimpatia Jane Goodall heshima ya kuheshimu (honorary doctorate) ya Maarifa ya Sayansi.
Japokuwa hii ni kwa uchache na maslahi ya Tanzania ila kwa dunia ni mtu aliheshimika haswa ana tuzo za heshima, Marekani, Uingereza, Japani, Uholanzi, Uhispania ,pia kimataifa (UN)
Huyu mama aliishi apumzike kwa amani
Ongezea nyama kidogo mkuu