Dkt. Kalemani: Marufuku kuuza mafuta yasiyo na vinasaba

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Dodoma, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amepiga marufu uuzaji wa mafuta ya Petroli, Dieseli, na Mafuta ya Taa yasiyo na vinasaba unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara nchini.

Dkt. Kalemani alitoa maagizo hayo Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kushtukiza ya kukagua vinasaba kwenye mafuta yaliyopo katika vituo vya kuuzia mafuta mkoani humo, iliyofanyika Aprili 20, 2021.

Katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja, Naibu Katibu Mkuu, Kheri Mahimbali na Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuberi wa wizara hiyo, pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka wa Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini( EWURA),Mhandisi Godfrey Chibulunje.

Dkt. Kalemani Alisema kuwa vinasaba vinadhihirisha viwango na ubora wa mafuta nchini.

β€œMaelekezo yangu kwa wauzaji wa mafua nchini ni lazima muendelee kuuza mafuta yenye vinasaba kwa sasa ili kujiridhisha na kiwango na ubora wa mafuta nchini, na kama mafuta hayana vinasaba ni marufuku kuyachukuwa na kuuza, kuna minongono katika baadhi ya maeneo kuwa kuna mafuta yanayouzwa ya aina hiyo, tutakayembaini tutachukua hatua stahiki, alisema Dkt. Kalemani.

Katika ziara hiyo, hakuna kituo hata kimoja kilichobaininika kuuza mafuta yasiyo na vinasaba.

Alieleza kuwa kwa sasa Shirika la Viwango nchini (TBS), ndiyo llililopewa kazi ya kupima na kuweka vinasaba katika mafuta yote yanayoingia nchini ili kudhibiti ubora na tayari kazi hiyo imeanza kufanyika.

Alisisitiza kuwa kuanzia sasa mafuta yote nchini yatakuwa yakipimwa na kuwekwa vinasaba na TBS na ikibainika kuna mafuta ambayo hana vinasaba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watendaji husika.

β€œTBS ni chombo cha serikali, kinachofanya kazi ya kudhibiti ubora na viwango ikiwepo wa mafuta nchini hivyo kuanzia sasa ndiyo kifanya kazi ya kupima na kuweka vinasaba kwenye mafuta yote nchini, endapo atatokea mwingine mtaelekezwa na serikali, alisisitiza Dkt. Kalemani.

Lengo la serikali kuipa TBS kazi ya kuweka vinasaba katika mafuta yote nchini ili kuokoa fedha za serikali zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa mwezi.
 
Siasa uchwara bana.

Mpaka sasa hao TBS hawajui hata hivyo vinasaba ni nini na vinawekwaje kwenye mafuta.

Halafu unasemaje unaokoa pesa za serikali wakati hiyo Tsh 17 iliyokuwa inalipwa kwa waweka vinasaba ni makato kutoka kwa wafanyabiashara wenyewe kwa kila lita ya mafuta??

Hiyo pesa inakuwaje tena ya serikali ?

Aisee
 
Suala la kudhibiti ubora lifanywe na TBS huwezi ukaweka kampuni binafsi ya kudhibiti viwango hata kama wanaolipia ni wafanyabiashara ya mafuta. Kulikua na mazingira ya upigaji hapo.
 
Suala la kudhibiti ubora lifanywe na TBS huwezi ukaweka kampuni binafsi ya kudhibiti viwango hata kama wanaolipia ni wafanyabiashara ya mafuta. Kulikua na mazingira ya upigaji hapo.
Kwani kuna mtu kalazimisha iwekwe kampuni binafsi wewe tikitimaji??
 
Mimi si ninajua vinasaba ni Deoxyribonucleic acid iliopo ndani ya cell na hii inayowekwa kwa mafuta na tbs ni gani tena!!
 
Suala la kudhibiti ubora lifanywe na TBS huwezi ukaweka kampuni binafsi ya kudhibiti viwango hata kama wanaolipia ni wafanyabiashara ya mafuta. Kulikua na mazingira ya upigaji hapo.
Mafuta yanakotoka huko na bandarini yanapimwa yako katika spec zake basi hizi zingine mbwembwe za kukusanya pesa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…