Dkt. Kalemani: Marufuku kuuza mafuta yasiyo na vinasaba

Dkt. Kalemani: Marufuku kuuza mafuta yasiyo na vinasaba

Mimi si ninajua vinasaba ni Deoxyribonucleic acid iliopo ndani ya cell na hii inayowekwa kwa mafuta na tbs ni gani tena!!
Hapo hadi wataalamu wa afya na msosi waje kunena
 
Dodoma, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amepiga marufu uuzaji wa mafuta ya Petroli, Dieseli, na Mafuta ya Taa yasiyo na vinasaba unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara nchini.

Dkt. Kalemani alitoa maagizo hayo Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kushtukiza ya kukagua vinasaba kwenye mafuta yaliyopo katika vituo vya kuuzia mafuta mkoani humo, iliyofanyika Aprili 20, 2021.

Katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja, Naibu Katibu Mkuu, Kheri Mahimbali na Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuberi wa wizara hiyo, pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka wa Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini( EWURA),Mhandisi Godfrey Chibulunje.
Huyu Kalemani aache ujinga ameambiwa ukiritimba wa Tanesco kuwaingizia watu umeme hajalisimamia hilo wala hajalifuatilia
 
Huyu Kalemani aache ujinga ameambiwa ukiritimba wa Tanesco kuwaingizia watu umeme hajalisimamia hilo wala hajalifuatilia
🤣🤣🤣 Viongozi wetu maigizo mengi sana
 
🤣🤣🤣 Viongozi wetu maigizo mengi sana
Nimemdharau sana huyu kichwa mbovu, watu wanampelekea malalamiko kuhusu mambo wanayofanya mameneja Tanesco wa mikoa yeye anatuma meseji kwa haohao wanaolalamikiwa badala ya kuwawajibisha
 
Nimemdharau sana huyu kichwa mbovu, watu wanampelekea malalamiko kuhusu mambo wanayofanya mameneja Tanesco wa mikoa yeye anatuma meseji kwa haohao wanaolalamikiwa badala ya kuwawajibisha
Nchi yetu inaongozwa na viongozi kama wanaongoza familia zao
 
Baada ya shabib kuwalipua na kampuni yao walikuwa wanajilipa bilioni 7 kwa mwezi wamerudisha jukumu kwa TBS.
Shabib alimlipua mpaka huyo waziri na kuikataa hoja ya Waziri... [emoji23] [emoji23]
 
Waziri kiboko utadhani mafuta yanachotwa mtaani kumbe yote yanatoka bandarini ambako wao ni rahisi kukagua kuanzia huko sio mtaani...ni sarakasi za uongo tuu..
 
Elezeni hiyo vinasaba kwa kingereza chake tuelewe, style za kutohoa kiboya mnapoteza technical meaning sasa genes ni vinasaba pia, confusion
 
Back
Top Bottom