Mbunge wa zamani wa Nzega Vijijini na aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, amesema hana kinyongo wala malalamiko yoyote baada ya kushindwa kurejea bungeni, akisisitiza kuwa anawaheshimu na kuwashukuru wananchi pamoja na wanachama wa CCM kwa kumfanya awatumikie kwa miaka 15.
"Sina kinyongo hata chembe kwa wananchi wenzangu na wanachama wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi wa Nzega ama wa Nzega Vijijini kwa sasa, na hata viongozi wote wa ngazi zote za Mkoa, ngazi za Taifa, Kwa sababu kuhudumu kwa miaka 15 kwenye Bunge la nchi yako ni heshima kubwa sana."
Akizungumza kwenye mahojiano na Wasafi Media mnamo Septemba 21, 2026, Kigwangalla alieleza kuwa maamuzi ya wanachama na vikao vya chama ndiyo yaliyoonyesha mwelekeo, na kwake yeye kuitumikia nchi kwa muda mrefu huo ikiwemo kushika nafasi za uwaziri na uenyekiti wa kamati mbalimbali za Bunge ni heshima kubwa