johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Waziri wa utalii Dkt. Kigwangalla amesema wananchi wana haki ya kikatiba ya kuisema na kuikosoa serikali iliyopo madarakani. Dkt Kigwangalla amesema yeye haoni tabu kukosolewa au kutukanwa mitandaoni kwa sababu hiyo ndio siasa yenyewe.
"Wizara hii hata nilipokuwa mbunge kabla sijateuliwa niliifahamu kuwa na matukio mbalimbali ya kutisha, ikifika wakati wake wa bajeti walikuwa wakiisubiria kwa hamu kuchangia na kulipua mabomu na kuwashambulia mawaziri na mawaziri walikuwa hawadumu muda mrefu"
“Hata nilipoteuliwa niliambiwa sidhani kama nitafika mbali, wakati nilipoteuliwa niliulizwa nitafanya nini ili nisitumbuliwe kama wengine, niliwaambia waniache nifanye kazi tutakutana mwaka 2020 ndio hii sasa nakwenda miaka miwili hadi mitatu sasa"
"Rais Dkt John Magufuli akikupenda sana atakutoa kwa heshima atakusemea mambo mengine hayo mengine hayasemi na ukiona upo kwenye wizara muda mrefu ujue yeye na vyombo vyake wanakufuatilia hadi wanajiridhisha huyu mtu hapigi pesa"
Dr Kigwangalla alikuwa akihojiwa katika studio za Clouds na watangazaji Babie Kabae na Sam Sasali.
Ametia nia ya kutetea jimbo la Nzega vijijini
Chanzo: Clouds 369