Dkt. Koboko tosheka na majukumu ya Udaktari, mwache Mfamasia kwenye eneo lake la madawa

Umeongea vizuri ,ila elewa hii ADDO imegeuza watu kuwa ma priscriber ,and most pharmacy ndo KAZI Sasa Kama hujajua fanya utafiti, that's

Hoja ya prof ina mashiko, mfamasia hawepo na dr awepo, vinginevyo pharmacy na hivyo viduka vya dawa muhim vifungwe , serikali ije na pharmacy zake au halmashauri husika Ili kulinda afya za watanzania, yanayofanyika kwenye hizi duka sijui phamarcy ni makubwa Sana kuliko unavyofikili,
Labda upasuji ndo umebakia kule, that's drugs resistance ipo juu,
 
Sasa Kama cheti Cha mfamasia kipo pale Chato Kama picha ya rais ila yeye mwenye cheti yupo Tanga, effect yake ni nini? Acheni umiza afya za ndugu zenu kisa vipande vya fedha,

Nishauri wizara ya afya ikaunde kamati ya siri chunguza pharmacy nchi nzima alafu wakikuta cheti Cha mfamasia pale watake onana nae hapo KWa hapo watabaki kucheka, hawapati mtu kwenye mia watapata watano

Acheni michezo michafu,na sasa mnataka wapanda madactari vichwani acheni izo
 
Kwa ulivyoeleza hapo na.hoja za Dr koboko mie pia naungana nae moja kwa moja maduka ya dawa yauzwe na madaktari ila watu wa famasia watengeneze dawa

Hoja ni. Hii kuna watu wengi wananunua dawa famasi bila kupata cheti cha daktari na kama wafamasia hawajasoma magonjwa hivyo wanatoa dawa kwa hisia ndo maana tunapata usugu wa dawa sanaa

Hoja ni nzito mnoo muhimu wafamasia wajikite kwenye kutengeneza dawa na kazi ya kuuza dawa na kutoa dawa ibaki wa madaktari wa binadamu

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Dr atauzaje kitu asichokijua? Anajua vitu vilivyopo ndani ya dawa?
 
Mkuu 'ZALENDA', hiyo siyo pharmacy ambako hupewa dawa bila kuwa na cheti cha daktari. Kwa kufanya hivyo nawe unashiriki katika uhalifu unaofanywa na hao wanaotoa dawa kwa mgonjwa kabla mgonjwa hajaenda kumwona daktari.

Ni wajibu wako kuzuia uhalifu huo.

Nayasema haya kwa sababu sitaki taaluma ya Pharmacy ionekane kama ni taaluma ya kijambazi. Wanaofanya hayo uliyoeleza wewe, hata kama wamehitimu kama Famasia, wanakiuka taratibu za kazi zao na wanavunja sheria za nchi. Hiyo siyo Famasi.

Na hili la kutumia vyeti ukutani nalo ni uzembe wa taasisi inayohusika katika kusimamia fani ya Famasia kuhakikisha wahusika wanafanya kazi zao kama inavyotakiwa na sheria.

Usicchukulie na kuhukumu fani nzima ya Famasi kwa makosa ya wanaofanya shughuli zao nje ya taratibu za fani husika.
 
Unasema hivyo kwa sababu hujaangalia madhara ya daktari kuuza mdawa na kuwa tabibu wakati huo huo.

Waliotenganisha wajibu huo na kuweka sheria kabisa hawakuamka tu siku moja wakafikiri kama unavyofikiri wewe hapa.

Unachokiona wewe ni uvunjifu wa sheria unaofanywa na hao wanaouza dawa holela huko Pharmacy. Suluhisho siyo kupeleka huduma hizo ambako kutakuwepo na matatizo zaidi ya yaliyopo sasa. Suluhisho, himiza vyombo vilivyopewa majukumu ya kuhakikisha fani hizi za kumhudumia mgonjwa zinafanya kazi zao kwa kufuata taratibu na sheria zinazozihusu.
 
Unatakiwa uelewe pia mfamasia haruhusiwi kumpa mgonjwa dawa bila cheti cha daktari. Lakini imekuwa ni kasumba ya wafamasia wengi kutoa dawa bila prescriptions toka kwa daktari jambo ambalo ni makosa
kiafya na kitaaluma.

Rai kuu ya Koboko ni Mfamasia hapaswi kutoa dawa moja kwa moja Kwa mgonjwa kwani hiyo si taaluma yao, ila wanafanya hivyo kwa muongozo wa daktari aliye muona mgonjwa husika.
Hapo utaona kabisa daktari halazimiki kupata MAFUNZO ya namna yeyote ya utoaji dawa kwani kashajotosheleza hapo.

Sasa hivi eti daktari, CO au nurse huruhusiwi kuuza dawa kwani??
 
Pharmacy is a business of Pharmacist.Not doctors or Nurses.

Ova.

Kuhusu mfamasia kumpa dawa mgonjwa.Sheria inasema kabisa. Mgonjwa anapaswa kwenda pharmacy akiwa na cheti kutoka kwa daktari. Na inajulikana hivyo.
 
Sasa hivi eti daktari, CO au nurse huruhusiwi kuuza dawa kwani??

Wanauza kupitia umiliki wa hayo maduka, yaani wao wawe tu wamiliki halafu muuzaji mahususi anatakiwa awe Pharmaceutical Personell(Pharm Tech, Pharm Assistant au Dispenser)

Soma hiki kipengele 43(2) cha Sheria ya Famasi
 
Kuna dawa nyingi zinaweza kutolewa bila kuhitaji cheti cha daktari.
 
Madakitari njaa..ni janga kwa kada ya afya.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina uhakika yule ni professor maana ni mweupe kichwani kwa hoja zake.
 
Hakuna mafunzo yoyote anayopewa daktari kuendesha pharmacy, mpaka hapo inaonyesha hujui tofauti ya ADDO na pharmacy.

Na sio kweli eti mfamasia hajui mgonjwa huyu apewe dawa gani, huyo atakua sio pharmacist maana baada ya kusoma dawa na magonjwa mengine bado kuna kozi inayoenda mpaka semester 3 inaitwa therapeutics(wengine wanaita clinical pharmacy au pharmacotherapy) hii utajifunza vitu vingi kuhusu tiba. Utahusianisha disease and treatment na utadeal na cases kibao. Pamoja na hayo bado mfamasia sio substitute ya daktari na wala hawajawahi kudai wafanye hayo majukumu.

Unapotaka daktari na nesi wawepo pharmacy hapo unataka uigeuze iwe hospital. Mwisho utataka pawe na maabara, kitanda, chumba cha sindano n.k maana ndio vitendea kazi vyao.

Kama ulivyosema jamii forums ni kisima cha maarifa basi ni jukumu la kila member kupokea maarifa kutoka kwa wengine.

Ni jambo la kusikitisha kuona mwanataaluma mbobevu lakini anakosa weledi na kudhani anaweza beba majukumu ya fani tofauti na yake.

Kuhusu ADDO nadhani hata wewe ukiona scope yake utajua tu haikumlenga nurse wala daktari maana ni ndogo sana na ilikua ni temporary tu. Nchi ikikaa sawa zinaondoshwa zote.

Mwisho pharmacy ni zaidi ya pharmacology, kujua pharmacology sio kujua kila kitu kuhusu dawa. Ndio maana kila prescription lazima ipitie kwa pharmacist.

Kama umeshindwa kunielewa basi jaribu hata kutafiti nchi za wenzetu wanaendesha vp systems zao. Uone Uk, Germany, USA n.k wanaishije, Hakuna kitu kama hiki mnachopropose.
 
Naanza kukuelewa kwamba mfamasia sio mbadala wa doctor ,Na umeeleza utaratibu unavyotakiwa kuwa,lakini ndo mnachokifa huko kwenye pharmacy zenu na maduka yenu muhim chini ya iyo ADDO zenu?

Maana Ili kutatua tatizo lazima tuwe wakweli, je wagonjwa wangapi mmewai wanyima dawa kisa Hana cheti Cha dactari , hospitali za uma mgonjwa hawezi pata dawa pharmacy Kama Hana cheti za doctor vipi huko mtaani,

Leo pita maduka mawili na pharmacy bila cheti Cha doctor Kama hutopewa dawa, Sasa hayo mamlaka mnayatoa wapi?
Leo tunadanganyana hapa wakati sio kinachofanyika mtaani KWa faida ya nani

Napendekeza utaratibu wa kuratibu biashara yenu hii kuangaliwa upya na serikali, na hasa usimamizi wa biashara hii kuanzia wilaya mpaka juu usiwe chini ya usimamizi wa mfamasia peke yake bali uwe chini ya Tim mahalum,

Mwisho afya za watanzania zipo mikononi mwa Doctors, Hawa wafunzwa,pharcology, history taking, how to diagnos and the proper way to priscribe medicine for specific disease ,wasikae kimia lazima kutoa tamko la pamoja, kuhusu Ili vinginevyo afya za watanzania zinaelekea babaya kuacha swala la tiba mikononi mwa wafamasia,
 
brother wamiliki wa famasi sio wafamasia pekee kuna watu binafsi ambao hawana taaluma ya famasi na pia doctors kibao wanamilik famas unafikil hao doctors wanaomilik famasi hawaoni ilo tatzo la kuuzwa dawa bila prescription? ila Mfamasia ndo yupo accountable famasi kutoa elim kwa wasaidiz wake dawa gan zitolewe na prescription na zipi zisitolewe sasa like all other health professional sio wote watakua perfect kwa kufuata kiapo walichoapa na kutoa dawa inavotakiwa.
Pili sio kwel daktari pekee ndo anajukumu la kutunza afya za mgonjwa dunia nzma hapa daktari pekee hawez kufanya hvyo pekee bila msaada wa wataalam wengne wa afya
 
Hapa solution ni mamlaka za Afya kukazia utekelezaji wa sheria. Mgonjwa asipatiwe dawa bila prescription ya Daktari, kitu ambacho ni kigumu kwa wamiliki/wauzaji wa dawa kukikubali ukizingatia pharmacy ni biashara.

Azabu ziwe kali na madaktari wapewe mihuri ya kutoka kwenye mabaraza yao ili ikitokea ame malpractise iwe easily kupata trace .
 
Uvurugeni tu mfumo wa afya bila kutafakari kwa kina halafu muone madhara yake, lazima mjue kumhudumia mgonjwa mpaka apone ni chain ndefu kwenye suala la afya sasa jifanyeni tu na ujuaji wenu wa kutoa dawa kama ndo kitu cha muhimu sana, wakati kuna vitu vingi sana vya kuboresha. Halafu mkumbuke Tanzania hii ni kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…