Taasisi ya Mifupa-MOI
Senior Member
- Apr 15, 2025
- 118
- 214
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, amepongeza huduma za kibingwa na kibobezi zinazotolewa na Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, huku akihimiza kuendelea kuimarishwa kwa kampeni ya "Vaa Helmeti, Ubongo Hauna Spea" ili kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda ubongo dhidi ya majeraha yanayosababishwa na ajali.
Akizungumza Julai 8, 2026, baada ya kutembelea banda la MOI katika maonesho hayo, Dkt. Magembe alisema hatua ya MOI kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi karibu na wananchi imeongeza fursa ya kupata matibabu pamoja na elimu ya kinga. Alieleza kuwa majeraha mengi ya ubongo yanayopokelewa hospitalini husababishwa na ajali za barabarani, hususan ajali zinazohusisha waendesha pikipiki na abiria wa bodaboda ambao hawavai helmeti au hawazingatii sheria za usalama barabarani.
Dkt. Magembe alisema elimu ya kinga ndiyo njia bora ya kupunguza idadi ya majeruhi wa ubongo na athari zake kwa familia na taifa, akisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kutambua kuwa ubongo ni kiungo muhimu kisichoweza kubadilishwa pindi unapopata majeraha makubwa.
"Hongereni MOI kwa huduma za kibingwa na kibobezi mnazozitoa kwa wananchi. Mbali na matibabu, mna jukumu kubwa la kuendelea kutoa elimu kupitia kampeni ya 'Vaa Helmeti, Ubongo Hauna Spea'. Ubongo hauna spea, hivyo kila mmoja anapaswa kujikinga kwa kuvaa helmeti akiwa anaendesha au amepanda pikipiki, kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani pamoja na kufuata taratibu za usalama mahali pa kazi. Tukifanya hivyo tutapunguza kwa kiasi kikubwa majeraha ya ubongo yanayotokana na ajali," amesema Dkt. Magembe.
MOI imeendelea kutumia Maonesho ya Sabasaba kama jukwaa la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kinga dhidi ya majeraha ya ubongo, ikihamasisha matumizi sahihi ya helmeti kwa waendesha pikipiki na abiria, kufuata sheria za usalama barabarani pamoja na kuwahi kufika hospitalini pindi ajali inapotokea ili kuongeza nafasi ya kuokoa maisha na kupunguza madhara ya kudumu.
Katika maonesho hayo, wananchi wanaendelea kunufaika na huduma mbalimbali za kibingwa na kibobezi zinazotolewa na MOI, ikiwemo ushauri wa kitaalamu, uchunguzi wa afya na elimu kuhusu kinga, utambuzi na matibabu ya magonjwa na majeraha ya mifupa, ubongo, uti wa mgongo na mfumo wa fahamu.