Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli aomba kura mtandaoni

Wazalendo na wapenda maendeleo ya Tanzania tutamchagua JPM kwa kishindo.

October 28 kura zote za ndio ni kwa JPM

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
Utamchagua na nani?

Na kwa akili yako finyu tukuulize kwanini Wazalendo mmekosekana huko Twitter kumhakikishia Ushindi?

Mmemwacha Mzee wa watu anapigwa za Uso peke yake, mlivo wanafiki Ndivo mtakavomwacha siku amefikishwa Kisutu kwa mashtaka ya kuiba Mali ya Umma na kupoteza watu
 
Kinachowatesa nyie ni kufikiria mambo yataendeshwa kwa mazoea tena. Inajulikana wako maadui wa ndani na nje ya Taifa la Tanzania. Maadui wa ndani wanao mamluki wao kwenye mifumo ya uendeshaji nchi, bila kwenda kwa chenga za mwili huwezi fika. Vita ya ndani ndivyo inavopiganwa hivyo.

JPM aliye kwenda kumzika Mkapa wakati wa kurudi akatembea kwa Miguu kuvuka daraja la Mkapa na akapokea zawadi ya jogoo Mkiru, akatumbua wakutumbuliwa. Ndio unaleta propoganda zako za kilaghai hapa eti anaogopa.

Kwani mlipanga kufanya nini akiwa anafanya kampeni huko Kusini apaka ikuume hivi kwa yeye kutoenda mikoa ya kusini?

Wezi na Mafisadi waliozalishwa Tanzania awamu hasa za 3 na 4 mmegeuka kuwa maadui wa Taifa hili kwa kujitahidi kukwamisha serikali ya awamu ya 5. Nyie ni wajinga kabisa hamna hata akili. Kama nyie kipindi chenu mlisimama hamkukwama pamoja na kupinduliwa kwa pambio la chama. Vipi sasa mfikiri hawa wa awamu ya 5 watawaangalia tu ili muwafanye waonekane mbele ya macho ya Watanzania wameshindwa?

Mambo katika Taifa hili hayaendeshwi kwa mazoea tena, jueni hivyo na mkae mtulie. Unaweza kumuita JPM muoga, Rais aliye thubutu kuing'oa accasia london stock exchange? Licha ya vitisho mlivyokuwa mwaviendeleza kwa propoganda zenu uchwara?

Akaikoa nchi ya Tanzania kutoka kubadilishana dhahabu na misaada ya vyandarua vya mbu. Eti, eti, eti, katumwa na Bahima, huna hata aibu wala soni wewe, hujishtukii kutumika kama tambara la kufutia shombo. Umelipwa nini kinachokufanya kudhalilisha utu wako na heshima yako kiasi hiki? Mtu aliyetumwa na Bahima angezuia madini yetu yasiishie Rwanda na kwengineko? Angejenga ukuta Mererani.?Angehangaika na Bwawa lilolomshinda Nyerere ubunifu wa kulijenga na huku nchi iikiwa na raslimali tele za kuwanufaisha Amiri Jamal na wakina Sabudu? Waliomfuatia Nyerere nao wakajibaraguza kulijenga ili wachote raslimali zilizojaa selous wakishirikina na mabwana zao wazungu na waarabu, sijui wahindi wanao waamini na kuwanyenyekea kama miungu -idols.




 
Sio ajabu akaja kuiruka hiyo akaunti na kusema Polepole amemlisha maneno
 
ila wakati mwingine unakaa unahisi kuna watu wanam-frame mzee wa watu. maana jinsi mtu anaejiita Kigogo alivyojibu wa kwanza kama Madenge utadhani alikuwa na taarifa mapema kuna tweet ya mzee inakuja.

yote kwa yote kura yangu kwa Lissu. na hata Mzee namshauri achague Chadema kutusaidia kutuondolea uozo unaoitwa CCM katila nchi yetu.
 
Maendeleo yapi ndg?
Maendeleo hayawezi kuja pasipokuwa na miundombinu mizuri ya kurahisisha kazi za kila siku za kibinadamu. Ili binadamu aweze kuendelea anatakiwa kutengenezewa nyenzo rahisi za kuweza kumfikisha mahali anapostahili kwa mfano, barabara, shule, hospital n.k.

Hivyo maendeleo ni 1. VITU
2. WATU
Pasipo VITU hakuna maendeleo na Pasipo WATU hakuna maendeleo
 
MATAGA mkuje mtuambie tangu lini kwenye mitandao kumekuwa na wapiga kura? Kila siku mnasema JF, Tweeter, Fb hakuna wapiga kura kuna wapiga kelele!?
Ni kweli wapiga kura wapo kwenye box la kura ambalo CCM ndio magwiji wa zoezi hilo..

Iyena iyena iyena CCM nambari wani...

October 28th kura zote kwa Mzalendo wa nchi hii,CIC,na kiboko ya wala Rushwa.


JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Kila mtu ana kadi yake ya mpiga kura... haya maelezo yote ya kazi gani?
Tunahitaji kura yako Mkuu usifanye makosa uichukue kura yako uiweke kwa JPM waaaaaa.

October 28th ndio mtajua hamjui na mihemko yenu...kura zote ni kwa JPM.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Hata aombe wapi, hatumtaki. Yeye na watu wake wote. CCM lazima waelewe kuwa wamechemsha kumuweka huyu kwenye nafasi hiyo, bora hata wangempa Kingwendu tungemfikiria.
 
Tunahitaji kura yako Mkuu usifanye makosa uichukue kura yako uiweke kwa JPM waaaaaa.

October 28th ndio mtajua hamjui na mihemko yenu...kura zote ni kwa JPM.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
Kama utabahatika uibe kadi yangu ndio Pombe atapata kura yangu.

Mihemko ya NYAKWENYU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…