Mwishoni wa mwaka jana Dunia iliingia kiwewe baada ya kuripotiwa ugonjwa wa virus vya Corona huko Mji wa Wuhan Nchini China
Badae maambukizi yakaenea kwa kasi Ulaya hasa Italy na nchi jirani kama Spain, Ufaransa nk
Hatimaye Marekani, Brazil, Urusi na India ndo wamekuwa virana wa maambukizi ya virus vya corona sasa.
Marekani pamoja na Rais Donald Trump kufanya mambo makubwa ndani ya miaka yake minne tu lakini swala la kuzembea kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya Corona linatishia kuweza kurudi tena kama Rais kwenye ngwe yake ya pili
Barani Africa virusi vilivyoingia tu Nchini Tanzania kupitia Rais wetu Dr John Pombe Magufuli akaja na maazimio mawili ambayo Dunia nzima haikumuelewa.
Pale aliposema Tufunge kama Taifa kwaajili ya maombi kwa Mungu na pili kuhoji ofisi ya maabara ya Taifa jinsi gani wanavyopima sampuli vya virus vya Corona.
Dunia ilitucheka sana na majirani zetu wakatubeza kiasi kwamba Gazeti moja nchini Kenya lilisema Magufuli ni "Kichaa na kina Bill Gates wakatabiri kwamba Africa muda mrefu maiti zitakuwa zinaanguka barabarani.
Kamanda wa vita na Jemedari Mkuu Kilongora Dr John Pombe Magufuli akaziba Masikio na kutoa tamko kwamba hii ni vita kwahiyo kila mtu apambane kivyake
Hatimaye chini ya Dr John Pombe Magufuli tuliishinda Covid 19 kwa 100% ndani ya muda mfupi sana na Dunia kuanza kutushangaa imekuwaje Rais Magufuli ameiishinda Covid 19
Rais wetu Dr John Pombe Magufuli amefanya mambo makubwa mno ndani ya miaka mitano kiasi kwamba sina mashaka na kushinda tena tarehe 28 October 2020
Lakini hili ya virusi vya Corona limeonyesha Tanzania tuna kiongozi mahiri,jasiri na zaidi mwenye maamuzi magumu kwa ustawi wa Taifa letu
Shime wa Tanzania wote tarehe 28 October 2020 kwa pamoja wale wote ambao tumejiandikisha tuende kwa ari kubwa kumpa kura za ndio mgombea kupitia Chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli
Week ijayo ntaeleza sababu zingine lukuki ambazo zinamfanya Dr John Pombe Magufuli kuendelea kuongoza Taifa hili miaka mingi ijayo zaidi ntajika kwa mambo ya maendeleo ndani ya miaka mitano iliyopita
YABISO CANIDAA?
CANDINDAA DR JOHN POMBE MAGUFULI OCTOBER 28 2020
Alex Fredrick
Dar es salaam Tanzania
View attachment 1597682View attachment 1597685View attachment 1597690