Haki ni pamoja na usawa, huwezi zungumzia haki wakati usawa hakuna, yani wafanyakazi wawe na mishahara mikubwa wakati wanafunzi wanakaa chini, wawe na laptop wakati hatuna maabara, mishahara yenyewe ikiwa mikubwa watashindwa kujenga na kununua magari kwasababu miundombinu ya kuendesha magari itakuwa mibovu, watashindwa kusafirisha vifaa vya ujenzi kwani gharama itakuwa kubwa sana kutokana na usafirishaji ndio maana tunajenga reli, mabwawa ya umeme n.k
Sent from my Infinix X650B using
JamiiForums mobile app
Katika yote uliyo yaorodhesha hakuna hata moja linalo husiana na usawa. Mfano wa wafanyakazi kutoongezwa mishahara/kutopandishwa madaraja havihusiani na wanafunzi kukaa chini.
Usawa ni labda ungetolea mfano wa mwalimu kutokulipwa kwa wakati achilia mbali mshahara husiokidhi majukumu ya mwalimu, na wakati huo huo kwa mbunge ukiondoa mshahara posho yakuhudhuria kikao pia analipwa kwa wakati, yaani akisaini kuhudhuria kikao tu 340,000 inamuhusu. Hapa ndio tutazungumzia kukosekana kwa usawa.
Mengine yote yanabaki kuwa haki.
Mwanafunzi kukaa chini ama kwenye dawati bado mwalimu analo jukumu lakumfundisha, hivyo ni haki ya mwalimu kuongezewa mshahara/kupandishwa daraja.
Walimu hawajapandishwa mishahara/madaraja, je wanafunzi wote wanakaa kwenye madawati?
Mishahara/madaraja havijapandishwa je kunatumika laptop?
Mishahara/madaraja havija pandishwa je tuna maabara ngapi za uhakika?
Kama kutoongezwa mishahara/kupandishwa madaraja ni kwa ajili ya maabara kwa nini vipimo bado vinatuambia papai na mbuzi vina corona?
Watu hawatoshindwa kujenga kwa sababu yakuongezwa mishahara, badala yake wameshindwa kujenga kutokana na kutoongezewa mishahara na kodi hisiyo rafiki kwenye vifaa vya ujenzi.
Watu hawatoshindwa kununua magari ndani/nje ya nchi kwa sababu yakuongezewa mishahara ama miundombinu, badala yake watashindwa/wameshindwa kwa kutoongezewa mishahara na mfumo wa kodi/ushuhuru husio rafiki.
Maendeleo ya watu ndiyo yanayo zalisha maendeleo ya vitu. Kwa mfano reli ya Tanga - Korogwe - Moshi adi Arusha ni maendeleo ya vitu, lakini kwa kuwa watu walikosa maendeleo reli ile ilisimama kwa miaka takriban 26 bila kutumika. Leo hii tumetumia fedha nyingi kuikarabati lakini mishahara ya watumishi haija panda (watu hawana maendeleo). Je miundombinu hii itakuwa na faida gani kwa mwananchi?
Haki yakupanda misharaha kwa wafanyakazi ndio chachu ya maendeleo ya watu na vitu.